728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, July 26, 2016

  TUZO ZA UBORA KIMATAIFA YA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA (TCAA)

  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (katikati) baada ya kukabidhiwa  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa na Raisi wa kampuni ya Otherways, Charbel Tabet inayoendesha mashindano hayo, jijini Rome Italy.

  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepokea tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi ubora wa kimataifa, jijini Rome Italy Julai 25, 2016.

  Kutolewa kwa tuzo hiyo kunafuatia mashindano yaliyohusisha zaidi ya makampuni 300 duniani ambayo yamesajiliwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) na kupitia mchakato wa kupigiwa kura na hatimaye kupata washindi.

  Meneja wa udhibiti wa viwangoTCAA, Magesa Sarota akielezea kuhusu tuzo hiyo alisema pamoja na mambo mengine mashindano hayo yanaangalia kampuni husika ni kwa namna gani inahakikisha inaendelea kutoa huduma zenye viwango katika masuala ya Uongozi pamoja na kuwa na mifumo inayohakikisha huduma wanazozitoa zinakidhi viwango.

  Tuzo hiyo ya TCAA ilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari kwa niaba ya Mamlaka. Kupokelewa kwa tuzo hiyo ni heshima kwa Mamlaka na ni motisha ya kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya wa kimataifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TUZO ZA UBORA KIMATAIFA YA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA (TCAA) Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top