728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 27, 2016

  Tanzania yazidi kupaa matumizi ya simu za mikononi


   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa akizungumza kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)  unaoendelea jijini Dar es Salaam ukifahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa mawasiliano ya simu za mikononi.

   Mkurugenzi Mkuu wa GSMA Bw Mats Granryad, akizungumza kwenye mkutano huo.

   Mkurugenzi wa GSMA Afrika Bw Mortimer Hope akizungumza kwenye mkutano huo.
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo.

   Mkurugenzi wa GSMA Afrika Bw Mortimer Hope akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana nana ripori hiyo.

  Tanzania ni miongoni mwa mataifa manane barani Afrika ambayo yana soko kubwa la simu za mikononi, ripoti  mpya ya utafiti  iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam imebainisha.
   
  Kwa mujibu wa ripoti hiyo  ijulikanayo;  ‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ iliyozinduliwa  kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)   unahofahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa aina hiyo ya mawasiliano, Tanzania  imeungana na mataifa ya Nigeria na Ethiopia ambayo  kwa utatu wao yanachukua zaidi ya theluthi moja  ya soko la aina hiyo ya mawasiliano barani Afrika.
  Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya  watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga  na huduma ya simu za mikononi  huku kukiwa na idadi kubwa ya watumiaji wa aina hiyo ya mawasiliano wanaohamia kwenye huduma ya internet inayopatikana kwenye simu zao, utafiti mpya uliofanywa na na Umoja wa wadau wa Mawasiliano ya simu za mikononi  Duniani  ujulikanao kama GSMA umebaini.
  Ripoti hiyo pia iliangazia mchango wa sekta ya mawasiliano ya simu hizo kiuchumi, ikiwemo ajira, ufadhiri kwa umma (Public Funding) pamoja na mchango wa mawasilian hayo katika ukuaji wa digitali na ushirikishwaji wa kifedha.
  “Zaidi ya watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga na huduma ya simu za mikononi, hatua ambayo si tu inawaunganisha bali pia inatoa fursa kwao kuweza kupata huduma nyingine kama vile huduma za afya, utambuzi wa kidigitali na huduma za kifedha,’’ alibainisha Mats Granryad, Mkurugenzi Mkuu wa GSMA. “Uhamiaji wa ghafla kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu miongoni mwa watumiaji  inatoa fursa mpya kwa watumiaji, biashara, serikali na kukuza mzunguko ambao mwaka jana uliongeza zaidi ya dola bilioni 150 kwenye uchumi wa bara la Afrika,’’
  Uwekezaji kwenye mtandao (Network) na simu za kisasa (Smartphones) kunachochea uhamiaji zaidi kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu.

   Ripoti hiyo imebaini kuwa kulikuwa na watumiaji milioni 557 wa simu za mikononi kote barani Afrika mwishoni mwa mwaka 2015, sawa na asilimia 46 ya idadi ya watu waliopo kwenye bara hilo na hivyo kufanya bara la Afrika kuwa la pili kwa ukubwa lakini lenye upenyaji hafifu wa aina hiyo ya mawasiliano duniani. Masoko makubwa ya simu za mikononi barani Afrika ni Egypt, Nigeria na Afrika ya Kusini  ambayo kwa pamoja yanachukua takribani theluthi moja ya jumla ya watumiaji wote barani humo. Idadi ya watumiaji inatabiriwa kufikia milioni 725 ifikapo mwaka 2020, ambayo ni sawa na asilimia 54 ya idadi ya watu wanaotarajiwa kuwepo kipindi hicho.
  Watumiaji wa simu za mikononi kwasasa wanahamia kwa kasi kwenda kwenye huduma za internet kutokana na ongezeko la mapinduzi ya internet na ongezeko la upatikanaji huduma nafuu za internet. Internet ya 3G/4G ilichukua zaidi ya robo ya watumiaji wa simu mwishoni mwa mwaka 2015, lakini inatarajiwa kuchukua zaidi  ya theluthi mbili ifikapo 2020. Hadi kufikia katikati ya mwaka 2016 kulikuwa na mitandao (networks) ya live 4G ipatayo 72 kwenye mataifa 32 kote barani Afrika, nusu yake imezinduliwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Wakati huo huo idadi ya simu za kisasa barani Afrika inakadiriwa kuwa zaidi ya mara tatu ya sasa miaka mitano ijayo, zikiongezeka kutoka simu milioni 226 mwaka 2015 hadi kufikia milioni 720 ifikapo mwaka 2020.
  Mchango wa simu za mikononi kwenye  mapato ya nchi za Afrika (GDP), Ajira na kuongezeka kwa ufadhiri kwa umma (Public Funding)
  Matumizi ya teknolojia za simu na huduma zake kote Afrika kulizalisha dola bilioni 153 kwenye uchumi mwaka jana, sawa na asilimia 6.7 ya mapato ya nchi za bara hilo. Mchango huo unatarajiwa kuongezeka hadi kufikia dola bilioni  214 ifikapo 2020 (asilimia 7.6 ya mapato ya nchi (GDP) yanayotarajiwa) wakati mataifa ya Afrika yakiendelea kunufaika kutokana na ongezeko la uzalishaji na ufanisi ulioletwa na kushamiri kwa huduma za simu. Mtandao wa simu za mikononi barani Afrika ulichangia ajira milioni 3.8 mwaka 2015 na kutoa mchango wa dola bilioni 17 kwenye sekta ya umma kupitia jumla ya kodi. Idadi ya ajira zilizozalishwa na sekta hii inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia milioni 4.5 ifikapo mwaka 2020 huku mchango wa kodi unakadiriwa kuongezeka hadi kufikia dola bilioni 20.5.
   Ripoti hiyo inaelezea ni kwa namna gani simu za mikononi zinachochea ubunifu kwenye ujasiriamali  barani Afrika. Watoa huduma za simu wamekuwa wakisaidia ujasiriamali kwa kuwezesha uwepo wa huduma kama zile kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu, huduma za malipo kwa njia ya simu na nyingine nyingi.
  Teknolojia ya simu pia inachukua nafasi muhimu katika kukabiliana na changamoto za kijamii barani Afrika ikwemo kutoa utambuzi wa kiofisi, upatikanaji wa huduma ya internet pamoja na kutoa huduma za kifedha kwa wanajamii. Idadi ya watu waliojiunga na huduma ya internet kupitia simu barani Afrika imekuwa mara tatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kufikia milioni 300 mwaka 2015, sawa na robo ya idadi ya watu wote barani Afrika.Ongezeko la watu milioni 250 linatarajiwa kuingia kwenye matumizi ya internet ifikikapo mwaka 2020, na kufanya jumla iwe watu milioni 550 (asilimia 41 ya idadi ya watu inayokadiriwa wakati huo)
   “Athari za mabadiliko chanya kwenye sekta ya simu yanaonekana kwa kina zaidi barani Afrika kuliko sehemu nyingine yoyote barani Afrika; Sekta ya simu za mikononi barani Afrika ipo mstari wa mbele katika kusaidia kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa,’’ aliongeza Granryd. “Tunajikita katika kuandaa baadae nzuri kwa wananchi na biashara kote barani Afrika, kutoa huduma muhimu za mawasiliano, ajira bora,  fursa za kiuchumi, uzalishaji zaidi pamoja na ushindani,’’
   Ripoti mpya ya ‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ ipo chini ya idara intelijensia ya GSMA. Ili kupata ripoti kamili pamoja na taarifa nyingine, tafadhari tembelea: http://www.gsma.com/mobileeconomy/africa/.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Tanzania yazidi kupaa matumizi ya simu za mikononi Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top