728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, July 12, 2016

  SHIWATA kukutana na wenye nyumba, mashamba Mkuranga

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeitisha mkutano Jumamosi Julai 16,2016 kwa wanachama wake waliokamilisha nyumba zao, waliochangia ujenzi na waliogaiwa mashamba ili kujadili umuliki na maendeleo ya maeneo ya makazi na kilimo.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa mkutano huo utakaofanyika ukumbi la Chuo cha Splendid, Ilala \Bungoni utaanza saa tatu asubuhi ili kujipanga kuhamia kijijini kwao Mwanzega Mkuranga ambapo mpaka sasa kuna nyumba 185 ambazo tayari zimejengwa na wanachama hao kwa njia ya kuchangishana.

  Alisema wanachama ambao watahamia katijka nyumba zao watapewa ekari moja bure kwa ajili ya kulima na ufugaji kwa ajili ya kuwaendeleza wajasiriamali wa SHIWATA.

  Taalib alisema SHIWATA inakusudia kuwapokea wadau na wajasiriamali mbalimbali wa sanaa na michezo ambao watapatiwa fursa ya kujiunga na mtandao huo kwa gharama ya sh. 100,000 kuanzia Julai 18, 2016 hadi Septemba 30,2016 itawafaidisha wajasiriamali na wadau hao kupata eneo la makazi lenye ukumbwa wa mita 35 kwa 35 pamoja na ekari moja bure kwa wale ambao wamejenga na kuhamia.

  Alisema kwa upande wa shamba, SHIWATA inampango maalum wa kuendesha kilimo cha pamoja kutumia wataalamu wa kilimo wawilaya ya Mkuranga ili kufanikisha mradi wa kilimo kwa njia ya kuchangiana.

  Pia SHIWATA inakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga shule, hospitali pamoja na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali ambapo baada ya kujiunga na mtandao huo watapewa maeneo bure.

  Mwenyekiti Taalib alisema Ujenzi wa awamu ya sita unatarajiwa kuanza Julai 30 mwaka huu na nyumba zitagaiwa kwa wanachama watakaokuwa wamekamilisha michango ya ujenzi wa nyumba zao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHIWATA kukutana na wenye nyumba, mashamba Mkuranga Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top