728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, July 15, 2016

  SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MASHRIKA NA TAASISI MBALIMBALI ZINAZOTOA MISAADA YA MAFUTA MAALUM (VILAINISHI)  Waziri wa afya jinsia watoto maendeleo ya jamii na wazee Ummy mwalimu akiongea na wafanyakazi wa hospital ya Mkoa wa Kagera(hawapo pichani)kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu.

  Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kagera
  SERIKALI imepiga marufuku kwa mashirika na taasisi mbalimbali zinazotaa misaada ya mafuta maalum(vilainishi)kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

  Waziri wa afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wakati akizindua jengo la wodi ya wazazi lililojengwa kwa ufadhili wa shirika la jhpiego kwenye hospital ya Mkoa wa Kagera.

  Ummy alisema kuwa mashirika au tasisi zinatazokuwa zinatoa huduma za kupinga vita juu ya maambukizi ya ukimwi kabla ya kuwafikia walengwa waanzie kwa wakuu wa Mikoa husika na kutoa maelezo ya kina ni kitu gani wanaenda kufanya.

  "Serekali na viongozi wa dini kila siku wanapiga vita masuala ya ushoga na ukahaba,lakini kuna baadhi ya mashirika yanahamasisha ushoga kwa kutumia mbinu za kutusaidia,hivi tunajenga Taifa gani la baadae linalokiuka utamaduni wake"alisema

  Alisema serekali hii haiwezi kulea masula ya mapenzi ya jinsia moja(ushoga)na wala hawatawapa nafasi mashirika yanayohamasisha mapenzi ya jinsia moja kutoa misaada.

  "Kuanzia leo serekali inapiga marufuku mashirika na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na usambazaji wa vilainishi vinavyochochea mapenzi ya jinsia moja kwa madai ya kuwa wanapunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi"alisema

  Alisema kutokana na utafiti uliofanywa na wizara ya afya hivi karibuni unaonyesha kuwa wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja ni asilimia 40 na wanawake ni asilimia 37 kwa Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MASHRIKA NA TAASISI MBALIMBALI ZINAZOTOA MISAADA YA MAFUTA MAALUM (VILAINISHI) Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top