JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Serikali Kutenga bil. 15 kukuza ujuzi wa Vijana Nchini.

Share This
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama wa kwanza kulia akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kuwa mdhamini wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Mkurugenzi Mtendaji wa ARIS Bw. Sanjay Suchak wa kwanza kushoto wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama akizungumza na wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wadau kutoka wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Na Ally Daud-Maelezo
Serikali imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kuchangia kuinua uchumi wa nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo ili kukuza ujuzi wa vijana katika sekta mbalimbali kwa madhumuni ya kuwakwamua vijana katika uchumi.

“Tunatambua vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wan chi hapa tulipo mpaka kufika uchumi wa kati hivyo katika kila bajeti tutatenga bilioni 15 kuwawezesha vijana kiujuzi” alisema Bi. Mhagama.

Aidha Mhe. Jenista ameongeza kuwa Serikali imeanza kupitia na kurekebisha upya sheria itakayowawezesha  wafanya biashara kuweza kumiliki uchumi wa nchi ili kufikia malengo waliyojiwekea hadi kufikia 2020.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na maswala ya Bima (ARIS) Bw. Sanjay Suchak amesema kuwa anashukuru kuona serikali imeweka mkakati wa kupitia upya na kurekebisha sheria itakayowaruhusu wafanya biashara kumiliki uchumi kwani kwa hali hiyo itawezesha kundi hilo kushiriki katika masuala ya ujenzi wa uchumi wa nchi.

Naye Mwenyekiti wa Sekta binafsi Nchini (TPSF) Bw. Reginald Mengi amesema kuwa ipo haja ya  watanzania hususani wakulima washirikishwe kwenye semina mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi kwani asilimia 60 ya watanzania ni wakulima.

Mkutano huo wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji umeandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa lengo la kujadili jinsi ya kutumia fursa na kuwezesha nchi kukua kiuchumi limeanza Julai 21 na kumalizika 22 Julai mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad