JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RUSHWA YAPIGWA MARUFUKU KWENYE UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI.

Share This
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula ayataka Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kuepuka rushwa kutoka kwa wenye fedha kwa kuwapa upendeleo na kukandamiza wanyonge katika maamuzi yahusuyo migogoro ya ardhi.

Angeline ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini. Wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watu ambao huwapa pesa waendesha mashtaka na wenyeviti wa mabaraza ya Ardhi na nyumba ili kupindisha sheria.
   Naibu Waziri wa Ardhi, Dkt Angeline Mabula akiongea na watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akipekua mafaili ya hukumu za migogoro ya ardhi ili kujiridhisha kama haki inatendeka kwa wananchi wakati alipotembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
Baadhi ya watendaji na watumishi wa umma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula katika ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad