728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 21, 2016

  RIPOTI YA KIUCHUMI BARANI AFRIKA YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

  Ofisa Uchumi  wa Idara ya Afrika wa Nchi Zinazoendelea  kutoka Geneva (Unctad), Claudia Roethlisberger, akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam,jana. Kulia ni Ofisa habari Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah Vuzo.
   Ofisa habari Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah Vuzo,akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo ya maendeleo ya kiuchumi barani afrika. Kushoto ni Ofisa Uchumi  wa Idara ya Afrika wa Nchi Zinazoendelea  kutoka Geneva (Unctad), Claudia Roethlisberger.
  Mtafiti wa Shirika linalojishughulisha na masuala ya utafiti wa masuala ya uchumi (REPOA),Stephen Mwombela,akichangia mada katika mkutano huo.
  Wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi nchini wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa ripoti hiyo .

  ………………
  NA ELISA SHUNDA

  SERIKALI za Afrika zimeshauriwa kuchukua hatua ya kuzuia ukuaji wa madeni ya mataifa yao ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea kama iliyowahi kutokea miaka ya mwishoni mwa 1980 na 1990.Pia zimetakiwa kuongeza vyanzo vipya vya mapato kwaajili ya kugharamia maendeleo ya nchi zao.

  Kauli hiyo imetolewa jijini hapa jana na Ofisa Uchumi Idara ya Afrika,Nchi zinazoendelea ambaye ni mwakilishi kutoka Geniva, Claudia Reothlisberger, wakati alipokuwa akizindua Ripoti ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika.“Ripoti hii ya UNCTAD inayozinduliwa leo(jana) inayohusu Maendeleo ya Uchumi barani Afrika, lakini tufahamu imekuwa ikichapishwa kila mwaka kuanzia mwaka 2000,lengo likiwa ni kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na hasara ya uwezekano wa ushirikiano mkubwa wa kiuchumi na uchumi wa dunia kwa kufanya utafiti na uchambuzi sambamba na kujenga maridhiano na ushirikiano wa kiufundi,

  “Ripoti hii ambayo imezinduliwa chini ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo (UNCTAD), inasisitiza kuwa kukopa inaweza kuwa sehemu muhimu ya kuboresha maisha ya wananchi wa afrika lakini lazima kupata uwiano kati ya wakati wa sasa, na baadaye kwa sababu madeni ni hatari yanapokuwa sio endelevu” alisema.

  Aidha alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo ilibaini kuwa angalau dola za kimarekani bilioni 600 zinahitajika kila mwaka ili kufikia Malengo ya Maendeleo endelevu(SDGs) barani Afrika.Alisema licha ya ripoti hiyo kubaini pia kwa sasa nchi nyingi za afrika zimeanza kuondokana na utegemezi wa misaada rasmi ya maendeleo kutokana na kutumia vyanzo vyake vipya vya fedha na vyenye ubunifu lakini zinapaswa kuangalia vyanzo vya mapato vya nyongeza ambavyo vitasaidia afrika kufikia malengo yake.

  “Ripoti hii ambayo pia imepewa kichwa kidogo kuwa Mienendo ya Madeni na Fedha za maendeleo barani afrika ilionyesha kuwa zipo nchi kadhaa za Afrika zilikopa sana katika masoko ya ndani, na nchi hizo ni Nigeria, Ghana, Kenya,Tanzania na Zambia” alisema.Kwa upande wake Mchumi kutoka Benki ya Maendeleoa ya Afrika(AfDB), Prosper Charles alisema kuwa ni wakati sasa serikali kuwa macho na hatari za kukopa kutokana na masharti magumu yaliyopo katika kipindi hiki.

  “Ili kufikia malengo endelevu ya  ya millennia ni lazima serikali ijizatiti kutekeleza miradi yake haswa mipango yake ambayo itasaida kuondokana na hatari ya deni la taifa”alisema.

  Imeandaliwa na Shunda blog/elisashunda@gmail.com/0719-976633.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RIPOTI YA KIUCHUMI BARANI AFRIKA YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top