728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 25, 2016

  PSPTB Yaendesha Semina Kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara Muhimbili


  Msimamizi wa Ushauri na Utafiti (PSPTB), Amos Kazinza akitoa mada LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ugavi, Pindani Nyalile akiwa kwenye semina hiyo. Semina hiyo imelenga kutoa mafunzo kwa watendaji wa MNH ili waweze kuzingatia taratibu na sheria za manunuzi. Wakurugenzi na wakuu wa idara wa MNH wametakiwa kutoa haki wakati wa kutoa zabuni. Pia, wameshauriwa kutonunua bidhaa zilizopo chini ya kiwango.
  Baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa idara wakiwa kwenye semina hiyo ya siku tatu iliyoanza LEO katika hospitali hiyo.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akifuatilia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Jeremia akiwa katika semina hiyo LEO. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha akisikiliza jambo kwenye semina hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni katika hospitali hiyo, Dk Faraja Chiwanga akifuatilia mada kwenye semina hiyo.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: PSPTB Yaendesha Semina Kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara Muhimbili Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top