JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


PROF. MBARAWA AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA SIMU

Share This
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akifungua mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  wajumbe wa  mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360, wakifatilia mada jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa wananchi wa mjini na vijijini kutumia simu ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali za kimtandao zinazotumika hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa kimataifa wa chama cha kampuni za simu duniani GSMA mobile 360, Prof . Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano ya simu inawafikia wananchi wote ili kuwezesha kunufaika na huduma za simu za kisasa.

‘Ili wananchi waweze kupata maendeleo kwa haraka  na kunufaika na fursa za kimtandao katika masuala ya elimu, biashara, kilimo, afya na ustawi wa jamii kwa ujumla kunahitajika uwepo wa simu za kisasa zinazoweza kuruhusu mifumo ya kimawasiliano’, Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameitaja mifumo hiyo kuwa ni Elimu Mtandao, Afya Mtandao, Biashara Mtandao,  Kilimo Mtandao, Serikali Mtandao, Hali ya Hewa Mtandao ambavyo kwa pamoja  vitamhudumia mwananchi kwa ubora na wakati.
Amesisitiza kuwa serikali inashirikiana kwa karibu na kampuni  za mawasiliano ya simu ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha huduma za simu zinakuwa za uhakika na salama.

Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba mfuko wa Mawasiliano Vijijini unaendelea kunufaisha watanzania na mkakati wa kuhakikisha umeme unafika vijijini unaimarika sambamba na uwepo wa simu za kisasa za bei nafuu.

Takribani laini za simu milioni 39.9 nchini zinatumika katika huduma mbalimbali na hivyo huchangia uchumi wa nchi.

Waziri Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kukuza sekta ya mawasiliano hapa nchini ambapo hadi sasa tayari kilomita 18,000/- za mkongo wa taifa wa taifa wa mawasiliano zimejengwa hapa nchini.

 “Serikali itaendelea kudhibiti vifaa vya mawasiliano visivyo na ubora ili visiingie nchini na hivyo kuhakikisha watumiaji wa mitandao ya simu wanakuwa salama na wanaitumia mitandao hiyo kwa wakati wote’. Amesisitiza Prof. Mbarawa.

Mkutano huo wa siku mbili ambao pia umehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu wa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Bw. Thomas Luhaka ambapo pamoja na mambo mengine utajadili Changamoto mbalimbali na kuja na suluhisho na namna bora ya kuendeleza Sekta ya Mawasiliano duniani.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad