728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, July 19, 2016

  NSSF YACHANGIA MILIONI 50 HARAMBEE YA UJENZI MPYA WA LINDI SEKONDARI

  Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii NSSF Makao Makuu ikishirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Lindi Imechanga Jumla ya Shilingi Milioni 50 Kwa Ajili ya Kuchangia Harambee ya Kusaidia Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi Iliyoungua Moto Wiki Iliyopita.

  Kwa Kutambua Umuhimu wa Elimu kwa  Watoto Shirika Hilo Kupitia Mkurugenzi Mkuu Wake ,Aliewakilishwa na Meneja wa Mkoa Bi Nour Aziz Limetoa ahadi hiyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Majaliwa Kasim Majaliwa Alieongoza Harambee Hiyo Ambayo Ilihudhuriwa na Wadau Mbali mbali Akiwemo Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Mama Salma Kikwete.

  Katika Harambee Hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 80 Taslimu zilichangwa Huku Ahadi na Vifaa vya Ujenzi zikifikia Shilingi Milioni 640 Ambapo Katika Ujenzi Mpya Waziri Mkuu Ameagiza Kujengwa Jengo la Ghorofa litakalokuwa na Ofisi na  Madarasa.

  Katika Tukio Hilo la Moto,Jumla Ya Madarasa 9 na viti na Meza zaidi ya 300,Ofisi 4 na Vyoo Matundu 24  Viliteketea na Moto Uliotokana na hitilafu ya Umeme(PICHA Na Abdulaziz Video,Lindi).
   Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi,Bi Nour Aziz(kulia)akiwasilisha Ahadi ya Shirika Hilo la Kuchangia Milion 50 Katika Harambee Hiyo Iliyoongozwa Na Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majaliwa
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa Akimshukuru Bw Juma Namuna,Mkuu wa Kitengo cha Mafao Baada ya Shirika Hilo kuahidi Kuchangia Milioni 50.
   -Baadhi ya Vifaa Ikiwemo Saruji Vilivyotolewa na Wadau Mbalimbali Kuchangia Ujenzi mpya wa Shule ya Sekondari Lindi
  ,Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Mama Salma Kikwete Nae Akiwasilisha mchango wake katika Harambee Hiyo Huku Taasisi ya WAMA Ikihaidi Pia Kuchangia Vitabu Vya Shule Hiyo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NSSF YACHANGIA MILIONI 50 HARAMBEE YA UJENZI MPYA WA LINDI SEKONDARI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top