728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 27, 2016

  NEWZ ALERT:KOFFI OLOMIDE KUSOMEWA MASHITAKA YAKE BAADA YA KUKAA JELA KWA SIKU TANO KINSHASA

  Kama kawaida yake Globu ya Jamii imefanya jitihada za ziada ili kuachana na tetesi na maneno ya mitaani na kuwasiliana na maripota wake jijini Kinshasa ili kupata undani wa yanayomsibu mwanamuziki nguli wa DRC Koffi Olomide 'Mopao' kufuatia kisanga cha kutiwa mbaroni kwa kosa la kumshambulia mnenguaji wa bendi yake ya Quarter Latin aitwaye Pamela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya. 
  Ripota wetu amegundua  kwamba sio kweli Koffi Olomide tayari ameshahukumiwa kwenda jela miaka 18,  ama kama wengine wanavyosema miezi mitatu na wengine mwaka mmoja. Ukweli ni kwamba amepelekwa jela kwa siku tano kabla ya kufika tena mahakamani kujibu shtaka la kujeruhi kwa kukusudia (intentional injury) na kufanya fujo hadharani. 
  Baada ya kukamatwa leo Jumanne asubuhi nyumbani kwake Kinshasa alipelekwa mahakamani ambako amri ya kumweka jela kwa siku tano ikatolewa. 

  Shtaka kuu analokabiliwa nalo Mopao ni kumuumiza dansa wake wa kike na  kufanya fujo hadharani. Video zifuatazo zinaonesha Mopao alipokuwa akitolewa mahakamani na kupelekwa gereza kuu la Makala. Video ya chini ni wakili wake akieleza mambo yalivyo. Wanaojua Kifaransa kazi kwenu...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NEWZ ALERT:KOFFI OLOMIDE KUSOMEWA MASHITAKA YAKE BAADA YA KUKAA JELA KWA SIKU TANO KINSHASA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top