728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 13, 2016

  NEWZ ALERT: Msafara wa Dkt Harrison Mwakyembe wapata ajali, abiria wanusurika

  Habari zilizotufikia muda huu zinaeleza kuwa msafara wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye suti nyeusi) umepata ajali ambapo gari la DPP limepata ajali na kupinduka baada ya tairi la mbele kulia kupasuka wakati Dereva alipokuwa akijitahidi kuwekwapa watoto wawili waliokuwa wakivuka barabara ghafla na bila kuwa na tahadhari yoyote,ajali hiyo imetokea katika kijiji cha  Bwanga  na msafara unaelekea Chato kutokea Geita. 

  Taarifa zinaeleza kuwa gari hilo limeishainuliwa  na safari inaendelea huku
  Dereva na Abiria wote akiwemo Mkurugenzi wa makosa ya jinai Mhe. Biswalo Mganga na msaidizi wake wakiwa wametoka salama.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NEWZ ALERT: Msafara wa Dkt Harrison Mwakyembe wapata ajali, abiria wanusurika Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top