728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, July 31, 2016

  NAIBU WAZIRI MPINA AZITAKA RADIO ZA JAMII KUHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka Radio za jamii kuhamasisha usafiri wa mazingira nchini. Naibu Waziri Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa, mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

  Akitolea Mfano wa Radio Pride FM ya Mjini Mtwara yenye kupatikana katika frequencies 87.8 mjini Mtwara, ambayo imeanzisha kampeni ya usafi katika mkoa wa mtwara na wilaya zake kwa kufanya vipindi vya moja kwa moja na kutembelea wilaya za mkoa huo kufanya usafi wa mazingira kwa vitendo.

  Kwa Upande wake Bw. JUma Andrea Manager uzalishaji wa kituo hicho cha Radio, alisema kuwa lengo kubwa la kituo hicho kuhamasiha usafi ni kuunga mkono agizo la Mhe. Rais kwa kuwaweka pamoja wananchi, kuweka muamko na hamasa ili kujenga tabia ya kupenda usafi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa homa ya matumbo na kipindipindu.


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (katikati) akiangalia samaki katika soko ya wilaya ya Masasi akiwa katika ziara yake ya usafi na ukaguzi wa mazingira mjini Masasi, (kilia) ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bw. Selemani Mzee.
  Aliyeinama katikati akikusanya uchafu ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira Wilayani Masasi mwishoni mwa wiki.
  Bw. Benjamini Elias (kulia) Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Masasi akitoa taarifa na maelezo ya hali ya usafi wa soko la mji wa Masasi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina (kushoto), wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira mjini Masasi. (PICHA NA EVELYN MKOKOI)   Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.

  “Nimeona kuwa uchomaji moto misitu ovyo hapa kwenu umekithiri, uchomaji moto taka nao siyo njia nzuri ya uondoshwaji wa taka,hiyo kuwe na miondombinu rafiki kwa uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambae hatakuwa tayari kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa alisisitiza.”

  Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara ni muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa viwanda na usafi wa mazingira iliyohusisha pia ukaguzi wa machinjio ya mji wa Masasi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NAIBU WAZIRI MPINA AZITAKA RADIO ZA JAMII KUHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top