728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, July 17, 2016

  MKUU WA WILAYA MJINI ZANZIBAR AZINDUA MABARAZA YA VIJANA JIMBO LA MAGOMENI.

  4 
  Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas akizungumza na Vijana wa Jimbo la Magomeni katika uzinduzi wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni kabla yakulizindua rasmin Baraza hilo Julay 16, (kulia) Mbunge wa Jimbo hilo Jamal Kassim Ali na (kushoto) Mwenyekiti wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni Kassim Lila Msoma.
  5 
  Baadhi ya Vijana wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni wakimsikiliza Mgeni rasmin Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas hayupo (pichani) wakati wa uzinduzi huo.
  6 
  Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas na Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali wakiwapungia mkono Vijana kuwaaga baada ya uzinduzi wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
  1 
  Brasbend ya Chipkizi ikiongoza maandamano ya uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni katika shamrashamra za uzinduzi wa mabaraza hayo uliofanyika uwanja wa Magae Meya Mjini Zanzibar.
  2 
  Sabra Abdalla Amer akisoma risala ya vijana katika uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni.
  3Mwenyekiti wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni Kassim Lila Msoma akimkaribisha mgeni rasmin katika uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni, Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina  Joel Tomas (hayupo pichani).
  Na Maryam Kidiko/Maelezo Zanzibar. 17/07/2016.

  Mkuu wa Wilaya ya mjini Marina Joel Tomas amesema lengo la Serikali la kuunda Mabaraza ya Vijana ni kuona Vijana hao wanakaa pamoja ili kujadili mambo muhimu yanayowahusu na kupambana na changamoto zinazowakabili.Ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la vijana la jimbo la magomeni iliyofanyika katika uwanja wa magae meya wilaya ya mjini unguja.

  Mkuu huyo amefahamisha kuwa mabaraza hayo yatasaidia Vijana hao kuandaa Maandiko ya Miradi mbali mbali watakayoanzisha katika mabaraza yao kwa lengo la kujikwamua na maisha.Vile vile amesema kukaa pamoja vijana hao kutaiwezesha Serikali kupata urahisi wa kuwasaidia vijana kuliko kuwasaidia mmoja mmoja .

  Amesema kuwa Fursa za kuwapatia ajira Vijana hao Serikalini ni chache sana hivyo vijana hao wanapaswa kujiunga pamoja na kutafuta namna ya kujiajiri wenyewe.Aidha mkuu wa wilaya hiyo aliahidi kuwa serikali itakuwa karibu na Vijana hao sambamba na viongozi wa jimbo hilo ili kuzifanyia kazi changamoto zinazoyakabili mabaraza hayo.

  Nae Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ally alisema atashirikiana na Vijana ili kuleta maendeleo katika jimbo lake na kuungana na Serikali ya wilaya pamoja ili kuweza kuinuwa vipaji walivyokuwa navyo vijana katika jimbo lake .

  “Vijana wamejengewa jukwaa lao maalum la mabaraza ya vijana kuweza kujiendesha wenyewe, kujiajiri pamoja na kuweza kufanya shuhuli mbali mbali za kimaendeleo “Alisema Jamal .

  Mbunge Jamal alisema baraza hilo halipo kichama hivyo kila kijana anahaki ya kujiunga katika baraza ili asiweze kupoteza haki zake za msingi kama kijana .Hata hivyo amewataka vijana hao kuitumia vizuri nafasi hiyo waliyoipata
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MKUU WA WILAYA MJINI ZANZIBAR AZINDUA MABARAZA YA VIJANA JIMBO LA MAGOMENI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top