728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, July 19, 2016

  Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba awaagiza JKU kuanzisha kilimo mbadala badala ya kutegemea mpunga
  Na Masanja Mabula –Pemba 

  MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman amewaagiza wapiganaji wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kanda ya Pemba kuanzisha kilimo mbadala ili kujiongezea kipato na kuacha kutegemea kilimo cha zao la mpunga pekee . 

  Alisema , ni vyema jeshi hilo kujikita katika kilimo cha mboga mboga na matunda , ikiwemo matikiti na pili pili boga bidhaa ambazo zinavunwa kwa muda mfupi na soko lake linapatikana ndani ya Kisiwa cha Pemba .
  Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua zoezi la uvunaji wa mpunga kwenye bonde la Shinyanga katika Kambi ya JKU Msaani , na kuwataka maafisa kilimo wa Jeshi hilo kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga na matunda. 

  “Kilimo cha matikiti kinastawi vyema katika ardhi ya Pemba , na soko lake lipo kwani wanaozalisha kwa sasa hawajaweza kulitosheleza soko kutokana na kuwepo na watumiaji wa wengi ”alieleza. 

  “Wapo wakulima wa matikiti wanayozalisha kwa wingi hapa Kisiwani Pemba , lakini bado hawajaweza kulimudu soko la bidhaa hiyo , hi
  Akizungumzia zoezi la uvunaji wa mpunga , alisema uongozi wa JKU unapaswa kuandaa utaratibu maalumu ambao utawezesha kumaliza kwa wakati uvunaji ili zao hilo lisiharibiwe na mvua ambazo zinanyesha kwa baadhi ya maeneo ya kisiwa cha Pemba . 

  Mapema Afisa Mdhamini Wizara ya Nchi , Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , Juma Nyasa alisema zoezi la uvunaji wa mpunga katika bonde hilo linafanyika kwa kanda ya Pemba . Alisema kunahitajika nguvu za pamoja kati ya Serikali na taasisi zake na binafsi katika kufanikisha zoezi hilo , ambapo aliitaka Serikali ya Mkoa kuongeza nguvu kwa kupeleka nguvu kazi kuokoa zao hilo . 

  “Nguvu za pamoja zinahitajika ili kufaniakisha zoezi la uvunaji kukamilika kwa wakati , hivyo tunaiomba Serikali ya Mkoa kuongeza nguvu kazi kuokoa zao hili ”alifahamisha Nyasa . Bwana Shamba wa Jeshi la Kujenga Uchumi kanda wa Pemba Kapeni Said Abdalla alisema , bado katika mabonde yanayotumiwa na Jeshi hilo kwa ajili ya kilimo yanategemea mvua ambazo kwa msimu huu zilikuwa haba .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba awaagiza JKU kuanzisha kilimo mbadala badala ya kutegemea mpunga Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top