728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 18, 2016

  MKURUGENZI KISHAPU AKUTANA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI,AWATAKA KUWA NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA NA RASILIMALI ZA SERIKALI.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza na watumishi (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kujitambulisha leo ukumbi wa halmashauri. Kulia ni Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya hiyo, Wilson Nyamunda.
  Watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji, Stephen Magoiga wakati akizungumza kwenye mkutano wa kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais Dk. John Magufuli uliofanyika katika ukunbi wa halmashauri.
  Watumishi wafuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji, Stephen Magoiga wakati akizungumza nao kuzungumzia mikakati mbalimbali ya kujenga halmashauri.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kutambulishwa kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Ngabaganga Taraba pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (mbele kulia) akizungumza na wakuu wa idara ofisini kwake wakati wa makabidhiniano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo, Wilson Nyamunda ambaye pia ni mwanasheria wa wilaya hiyo (mbele kushoto). Wengine anayefuatia ni Mwenyekiti wa halmashauri, Boniface Butondo, Mchumi wa wilaya, Joseph Katobezi, Mhandisi Samson Pamphil na Mweka Hazina wa wilaya, Masatu Mnyoro.


   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga amezungumza na watumishi wa idara zote na kuwataka kutumia vizuri fedha za Serikali.Magoiga alisema halmashauri siyo kampuni ya mtu binafsi hivyo watumishi wanapaswa kuwa na matumizi sahihi ya fedha na rasilimali za Serikali hivyo kuepuka wizi na kujenga kutokuaminika kwa wananchi wanaowahudumia.

  Alihimiza uwazi katika utendaji huku akiahidi kuwa muwazi kwa watumishi wote na kuwa tayari kukosolewa pale inaponekana anakwenda kinyume na utaratibu wa utumishi wa umma.Kutokana na umuhimu wake aliipa meno Idara ya Ukaguzi wa Ndani katika halmashauri hiyo kuhakikisha kunakuwepo na matumizi sahihi ya fedha na kutoruhusu hati chafu.

  ”Audit querry (hoja za ukaguzi) ziibuliwe bila upendeleo pale ambapo pana matatizo katika mchakato wa malipo ya fedha kwa kusema hata kama ni mimi nihojiwe kwani tupo katika utawala wa sheria,” alisema.Aidha, alisema ukusanyaji wa mapato ni ajenda ya kitaifa na kuonya kuwa zoezi hilo lisiwe kero kwa wananchi na kuwa watendaji wanaohusika watoe elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa wao kulipa.

  Pia, aliwataka watumishi kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba, sheria, kanuni na miongozo yote ya Serikali huku akiwaomba ushirikiano na yeye akiwaahidi ushirikiano mkubwa.“Tuepuke kufanya kazi kwa upendeleo na tutoe taarifa kwa wakati na tuhudumie wananchi kwa wakati, taarifa hizo ziwe sahihi na tuache kufanya kazi kwa mazoea.

  “Rais hataki ‘business as usual’, mtu afike kazini kwa wakati na afanye kazi na si tu kuzunguka kwenye korido hadi muda wa kazi unaisha halafu ndiyo yeye anaanza kazi, tuwe na huruma kwa wananchi tunaowahudumia,” alisisitiza. Magoiga alizitaka idara kuwa na mpango wa kazi wa nini wanakifanya katika vipindi tofauti na kuhimiza ushirikiano miongoni wa watumishi wake badala ya mkuu wa idara kuwa ndiyo kila kitu.

  Aliitaka Idara ya Mifugo kwa kushirikiana na Idara ya Ardhi pamoja na Kilimo kuwatambua wakulima na wafugaji kwa kuwatengea maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli zao ili kuondokana na migogoro ya ardhi inayoweza kutokea kati yao.

  IMEANDALIWA NA ROBERT HOKORORO WA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MKURUGENZI KISHAPU AKUTANA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI,AWATAKA KUWA NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA NA RASILIMALI ZA SERIKALI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top