728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 18, 2016

  MBUNGE WA JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR ASHIRIKI UJENZI WA TENKI LA MAJI KATIKA JIMBO LAKE


  Mbunge wa Magomeni Jamal Kassim Ali akiponda zege katika ujenzi wa ujenzi wa mnara wa Tenki la maji uliopo Maskani ya Kula Jiwe Sogea, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake za upatikanaji wa Maji safai na salama katika Jimbo hilo.

  Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali (alievaa Shati la kijani) akishiriki ujenzi wa Mnara wa Tenki la maji katika eneo la Sogea Jimbo la Magomeni Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake za upatikanaji wa Maji safai na salama katika Jimbo hilo.

  Jioni yake Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali alitoa jezi kwa Tim 18 za mpira wa miguu na Netbol katika Jimbo hilo, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  Na Maryam Kidiko –Husna Sheha / Maelezo Zanzibar.

  Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ally amesema changamoto kubwa iliyokuwa inakabili jimbo hilo zimeaanza kupata ufumbuzi katika kila shehia ndani ya jimbo .

  Ameyasema hayo katika ujenzi wa mnara wa maji ndani ya shehia ya sogea jimbo la magomeni wilaya ya mjini unguja amesema ujenzi huo ni miongoni mwa ahadi walizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni . Amesema changamoto ya maji ilikuwepo kwa muda mrefu katika shehiya ya sogea jambo ambalo lilikuwa likirejesha nyuma maendeleo ya shehia hiyo.

  “Tumechukuwa juhudi kubwa na viongozi wenzangu kuanzia madiwani na muwakilishi ili kuona suala hili linakamilika haraka “ Alisema Jamal. Aidha amesema wameanzisha mradi wa visima vya maji sita katika jimbo hilo ili kuweza kupunguza tatizo la ukosefu wa maji ambalo ni muhimu kwa binaadam kuweza kupata huduma hiyo.

  Hata hivyo ametowa fursa kwa wananchi wa shehia hiyo kuweka kamati ya visima ili iweze kusimamia katika mambo mbali mbali yatayovikabili visima hivyo. Vile vile amefahamisha kuwa visima hivyo vya wananchi wote hivyo kila mwananchi anahaki ya kutumia na kuvitunza visima hivyo bila ya kufanya uharibifu .

  Pia amewaomba viongozi watakaochaguliwa kusimamia visima hivyo kuwa na hekma pamoja na busara ili kuweza kuepusha migogoro kwa wananchi wataopata huduma hiyo. Sambamba na hayo amewataka wananchi wa jimbo la magomeni mradi huo utapokamilika waweze kutoa michango ili kusaidia umeme ambao ndio utaweza kupatikana kwa huduma hiyo.

  Nae Ramadhan Mwadini mzee ambae ni miongoni mwa wa nanchi wa shehia ya sogea jimbo la magomeni amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa kuitimiza ahadi aliyoiahidi wakati wa kampeni. Amewataka viongozi wao wa jimbo kuendelea kutimiza ahadi mbali mbali walizozitoa ili kuweza kuleta maendeleo katika jimbo lao .

  Jumla ya visima vinne vimeshachibwa kati ya visima sita katika jimbo hilo na kila kisima kimegharimu shilingi milioni saba na laki tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MBUNGE WA JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR ASHIRIKI UJENZI WA TENKI LA MAJI KATIKA JIMBO LAKE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top