728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 18, 2016

  MADIWANI WA HALMASHAURI ZA KYERWA NA BIHARAMULO WAANZA MAFUNZO YA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA


  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deusdedith Kinawiro akifuyngua mafunzo ya siku nne ya Madiwani kutoka Hlamashauri mbii za Kyerwa na Biharamuo juu ya namna ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma (PS3) chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekali kupitia shirika ake la misaada la Kimataifa (USAID) ikishirikiana na serikali kuu.

  Mradi huo ulizinduliwa Julai 12 mwaka huu ambapo Halmashauri hizo mbii ndio zitatekeeza mradi huo mkoani Kagera kwa awamu ya kwanza.Kinawiro alisema anatarajio kuona mafunzo haya elekezi yanatumika kama ilivyokusudiwa, na waheshimiwa madiwani wanapata uelewa na maarifa kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu na majukumu yao katika kusimamia uendeshaji wa Mamlaka hizi. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali (Mstaafu), Shabaan Lissu akiwa na Mkuu wa Wiaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya madiwani yaliyofanyika mjini Bukoba leo. 
  Mwenyekiti wa Hlamashauri ya Kyerwa, Kashunju Runyogote (kushoto) akiwa na madiwani wenzake wa Kyerwa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.

  Baadhi ya Madiwani na Watendaji wa Hamashauri za Kyerwa na Biharamuo mkoani Kagera wakifuatilia ufunguzi huo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MADIWANI WA HALMASHAURI ZA KYERWA NA BIHARAMULO WAANZA MAFUNZO YA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top