728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 14, 2016

  MA DJ WATAKIWA KUJISAJIRI ILI KUIMARISHA TAALUMA YAO


  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni , Sanaa na Michezo akikabidhi vyeti vya usajili wa Chama cha Madijey nchini leo jijini Arusha kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Yusuph Juma kuashiria uzinduzi wa chama hicho rasmi.
  Naibu waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wmbura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madijey waliyo wanachama mara baada ya kuzinduliwa kwa chama hicho leo jijini arusha,(wanne kulia) ni Katibu tawala Mkoa Bw.Hargeney Chitukuro

  ……………………………


  Na Anitha Jonas – MAELEZO-Arusha.

  Wasanii wa wanofanya kazi ya u-dijey watakiwa kujisajili katika Chama kwa lengo kujenga misingi imara ya taalum hiyo.Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo alipozindua chama hicho rasmi katika mkutano wa wadau wa kisekta uliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa ambapo alikutana na wadau mbalimbali.

  “Kuanzishwa kwa chama hiki kuanashiria ni kwa kiasi gani wadau wa sekta ya sanaa wameelewa umuhimu wa kurasimisha kazi zao na hili litaongeza tija katika kujenga heshima ya kada hii ya madijey katika nchi yetu kama ilivyokwa nchi zilizoendelea”,alisema Naibu Waziri Wambura.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Madijey Bw.Yusuph Juma alisema wameamuo kuanzisha chama hicho cha madijey kwa kuwa sanaa hiyo imekuwa ikidharaulika kwa kiasi kikubwa imekuwa ikionekana kama siyo sekta rasmi bali ni uhuni .“Usajili wa madijey katika chama utazingatia vigezo vya taalum pamoja na leseni za udijey hii ni kwa lengo la kuimarisha sekta hii ili kuipa nguvu na kuifanya iheshimike kama kazi nyingine za kisana na sivinginevyo”,alisema Bw.Juma.

  Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo alisema madijey wengi nchini wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kulipwa ujira mdogo ukilinganisha na masaa wanayokuwa wakifanya kazi hiyo,hivyo kwa kupitia umoja huo wataunda muongozo utakaosaidia kuboresha mazingira ya malipo yao.

  Pia Bw.Juma ameiomba serikali kusimamia suala la madijey wote nchini kujiunga katika chama hicho kwa lengo la kuunda umoja wao utakowasaidia kupata fursa mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kutafuta namna ya kuongeza maslai yao.Hata hivyo uongozi huo umetoa shukrani kwa Serikali kwa ushirikiano uliyowapa katika kupitisha chama hicho ambacho kimesajili katika Baraza la Sanaa la Taifa .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MA DJ WATAKIWA KUJISAJIRI ILI KUIMARISHA TAALUMA YAO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top