728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 14, 2016

  Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii awaasa watanzania

    Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Kondo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR
   
  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Kondo amewaasa watanzania kuchukua tahadhari na watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwa kuwaaminisha wananchi kuwa maandamano na vurugu ndio demokkrasia na ukombozi wa umaskini wetu. 

  Kanali Kondo alisema kuwa watu wa aina hiyo ni wakuogopwa kama ukoma kwani ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu ambapo tunashuhudia vurugu, vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali duniani na madhara yake. 

  “watanzania tuchukue taadhari ya watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwani kumekuwa na watu wanaotuhamasisha ya kuwa maandamano na vurugu ndiyo ukombozi wa umaskini wetu hivyo tunapaswa kuchukua taadhari na kukataa hadaa hizo” alisema Kanali Kondo. 

  Vilevile aliongeza kuwa, roho mbaya imechangia taifa letu kudumaa kimaendeleo kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wetu wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara, watumishi wa umma, wasomi na wananchi wa kawaida. 

  Aidha,alifafanua kuwa katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais John Pombe Magufuli amechukua hatua ngumu ya kupambana na vitendo vya rushwa, ubadhilifu na ufisadi kwani kitendo hicho kimewaudhi mafisadi na mawakala wanaopotosha ukweli na kuendesha propaganda chafu dhidi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii awaasa watanzania Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top