728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, July 15, 2016

  JWTZ YAPANIA KUTOA WACHEZAJI TIMU ZA TAIFA

  Na Selemani Semunyu, JWTZ

  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeahidi kuhakikisha inatoa wachezaji katika Timu zote za Taifa kwa kuzingatia Michezo yote ikiwemo Soka ili kurejea zama zake za JWTZ kuwa kinara wa  Michezo Nchini na Kimataifa.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassor  Leo(Jana)wakati alipotembelea kambi ya wachezaji wa Timu teule za Jeshi zilizoweka Kambi ya Bavuai  iliyopo Unguja Zanzibar.

  “Hatuna sababu ya Wanajeshi Kutotoa mchango kwa Timu zote ikiwemo soka ukizingatia Michezo ni sehemu ya majukumu ya jeshi tofauti na sasa tumekuwa katika michezo mingine lakini kwa nini isiwe na soka” Alisema Meja Jenerali Nassoro.

  Alisema  Wachezaji wa Timu za jeshi wanatakiwa kutambua kuwa wanatarajiwa kwenda Rwanda kushiriki mashindindano ya Afrika mashariki si kuwakilisha jeshi bali kuwakilisha nchi hivyo wanapaswa kupigana kufa na kupona kuiletea nchi heshima.Meja Jenerali Nassoro amesema kutokana maandalizi ya mwaka huu hakuna sababu kukosa ushindi hivyo ni jukumu la wachezaji kutimiza matarajio ya Watanzania .

  “Mwaka huu ni mwaka wa kurejesha Heshima ya jeshi na taifa kwa kurudi na Ushindi kutokana na ukweli kuwa jeshi letu ni mahiri hata katika Nyanja za Michezo” Alisema Meja Jenerali Nasoro.

  Mkuu huyo wa Mafunzo na Utendaji Kivita aliwataka Wachezaji kuwa na NIdhamu,Weledi,na kujituma ili iwe kazi nyepesi katika kupata ushindi lakini kuwa bora katika mchezo husika kwa faida ya mchezaji mwenyewe.

  “Hakuna Sababu sasa tukose wachezaji katika Timu ya Taifa katika Soka na tuweze katika michezo mingine”

  Katika hatua Nyingine mkuu wa kambi hiyo Luteni Kanali Richard Mwandike amesema maandalizi yanaendelea vyema na hakuna majeruhi katika kambi hiyo huku mchujo wa pili ukitarajiwa kufanyika ili kupata wachezaji wachezaji hasa Watakaoenda Rwanda mwezi Agosti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JWTZ YAPANIA KUTOA WACHEZAJI TIMU ZA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top