728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 13, 2016

  Jeshi la Polisi lawaasa vijana kutumia michezo ya kuigiza kuelimisha jamii kuhusu kupambana na kuzuia uhalifu.

  Inspekta Salum Abdallah akitoa mada kuhusu vijana kutumia michezo ya kuigiza kuelimisha jamii kuzuia na kupambana na uhalifu nchini katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.(Picha na Shamimu Nyaki-WHUSM)

  Na Shamimu Nyaki WHUSM

  Serikali kupitia Jeshi la polisi limewaasa vijana nchini kushiriki katika michezo mbalimbali ya kuigiza yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupambana na kuzuia uhalifu.

  Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Inspekta Salum Abdalah kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi alipokuwa akitoa mafunzo kwa vijana kuhusu Umuhimu wa kutoa elimu kuhusu kuzuia na kupambana na uhalifu nchini kupitia michezo ya kuigiza.

  Inspekta Salum amesema kuwa miongoni mwa mikakati ya serikali ni kuwajengea vijana uwezo wa kuwa na tabia njema na kupata kipato cha halali kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya stadi za kazi kwa lengo la kuimarisha na kukuza uchumi, pamoja na kuwapa uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.

  “Ili kuwawezesha vijana kuwa na tabia njema na kuwa na maadili yanayotakiwa hatuna budi kuanzisha mbinu za kuwawezesha kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, ulinzi shirikishi na kuwepo kwa mipango thabiti wa kushiriki katika mafunzo, semina na warsha mbalimbali”. Alisema Inspekta Salum.

  Inspekta Salum ameongeza kuwa wananchi ,wadau pamoja na mamlaka zinazohusika na maendeleo ya Vijana, Michezo na ujasiriamali kuwahamasisha vijana ili waweze kujshughulisha na shughuli zinazoleta maendeleo kwa taifa na kujiepusha katika vitendo vya uhalifu.

  Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bw Ismael Mnikite amesema mafunzo hayo yamemuwezesha kuelewa umuhimu wa ulinzi shirikishi kwa vijana kwakua anaamini ndio wenye uwezo mkubwa wa kushawishi jamii kujiepusha na vitendo viovu.

  “Mafunzo haya yameniwezesha kuelewa umuhimu wa kuwa mfano kwa jamii kwani nitatumia elimu hii kupanua uwezo wa kutafuta miradi itakayoniwezesha kupata mikopo kutoka kwa wawezeshaji ili nisipate tamaa ya kujiingiza katika uhalifu”.Alisema Bw. Ismael.

  Mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana ili kuwasaidia vijana kuwa raia wema na kushiriki ipasavyo katika shughuli za ujasiriamali na ulinzi wa jamii kwa kutumia elimu na vipaji walivyonavyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Jeshi la Polisi lawaasa vijana kutumia michezo ya kuigiza kuelimisha jamii kuhusu kupambana na kuzuia uhalifu. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top