728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 18, 2016

  HIVI NDIVYO MAHARAMIA WA KAZI FEKI ZA WASANII WANAVYOIKOSESHA SERIKALI MAPATO KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA MAOFISA WA TRA WASIO WAAMINIFU

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Action Mart ,Alex Msama pichani kushoto akionesha stika halisi za TRA zinazotumika kuwekwa kwenye bidhaa mbalimbali zikiwemo kazi za wasanii wa Filamu na muziki na kulia akionesha CD ya Muimbaji wa nyimbo za injili Boniphace Mwaitege ambayo ni "FEKI" lakini imebandikwa stika halisi za TRA.
  Kufuatia kadhia hiyo,Msama ameeleza kuwa kumekuwepo na baadhi ya Maofisa wa TRA wasio waaminifu wakitumika kuhujumua Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuzitoa stika hizo halisi za mamlaka hiyo na kuwauzia maharamia wanaouza kazi feki za Wasanii zikiwemo pia na bidhaa mbalimbali hapa nchini,hali inayopelekea Maharamia hao kukwepa kodi ya Serikali sambamba na Wasanii wetu wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa.
  Msama amebainisha kuwa kufuatia uchunguzi wao walioufanya na kubaini hujuma hizo za kuidhoofisha Serikali kwa kukosa mapato yake, watachukua hatua ya kuufikisha uchunguzi huo kwa mamlaka husika,ili waliohusika kwa namna moja ama nyingine wachukuliwe hatua kali .

  Msama amempongeza Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kwa kazi aliyoifanya kutoka ofisini kwake na kuenda kwenye maduka mbalimbali yaliyopo katikati ya jiji Kariakoo kwa ajili ya kusaka na kubaini wezi wa kazi feki za wasanii,ambapo katika operesheni hiyo Mh Nape alifanikiwa kuyafunga maduka zaidi ya 40 yaliyokuwa yakidaiwa kuuza kazi feki ikiwemo na suala zima la kukwepa kopi.

  Amesema Jambo hilo limemtia moyo kama mpigania haki wa kazi za wasanii ambaye amekuwa akipambana kila siku ili wasanii waweze kufaidika na jasho lao na ataendelea na kazi ya kuhakikisha wezi wote wa kazi za sanaa wanashughulikiwa kisheria na kuwafanya wasanii nao wanafaidi jasho la mikono yao.
  Baadhi ya Vielelezo hivyo zikiwemo stika halisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),pamoja na CD Feki lakini imebandikwa stika za mamlaka hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HIVI NDIVYO MAHARAMIA WA KAZI FEKI ZA WASANII WANAVYOIKOSESHA SERIKALI MAPATO KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA MAOFISA WA TRA WASIO WAAMINIFU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top