728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, July 17, 2016

  HALMASHAURI YA KAHAMA YAASWA KUACHA KUCHUKUA TOZO ZISIZO NA UMUHIMU

  Anitha Jonas – MAELEZO,Kahama.

  Kahama.

  Halmashauri ya Kahama ya imeelezwa kuacha kuchukua tozo zisizo na umuhimu katika kipindi michezo yakunufaisha jamii.

  Kauli hiyo imetolewa jana Mjini Kahama na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akifunga mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Tushikamane yaliyohusisha Mikoa ya Kanda ya Ziwa na yamekuwa yakidhaminiwa na Kampuni ya Madini ya Acacia Buzwagi.

  “Ombi langu kwenu Kampuni ya Acacia Buzwagi muongeze mkataba wenu wa kuwezesha mashindano haya kwa kuwa kupitia msaada wenu vijana hawa wa Kanda ya Ziwa wanapata kipato ambacho kinawasaidia katika maisha yao ya kiuchumi”,alisema Naibu Waziri Wambura.

  Pamoja na hayo Naibu Waziri huyo alitoa rai kwa taasisi nyingine kujitokeza kusaidia mashindano hayo ya ili kuweza kuwafikisha mbali wanamichezo hao wenye uwezo mkubwa wa kufanya mchezo huo kufikia hata kiwango cha Kimataifa.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli Bw.Godfrey Mhagama alisema kwa mwaka huu kuna zaidi ya wachezaji 200 waliyoshiriki mshindano haya ombi langu kwa serikali ifatafute wadau watakao weza kusaidia kuendeleza vipaji vya vijana hawa kanda ya ziwa iliwaweze kuufanya mchezo huu kuwa ajira na kupata mafanikiwa makubwa kama wachezaji wa ulaya.

  “Wakazi wa Kanda ya Ziwa wa wanauwezo mkubwa katika uendeshaji wa baiskeli hii ni kutokana na utamaduni wao wa kutumia Baiskeli kama chombo cha usafiri”,alisema Bw.Mhagama.

  Naye Meneja wa Mgodi wa Acacia Buzwagi Bw.Asa Mwaipopo alisema katika mashindano hayo ya mwaka huu watatoa zawadi kuanzia mtu wa kwanza mpaka wa 30 na katika mashindano hayo wanaume watakimbia kilomita 156 na wanawake kilomita 80 na zawadi ya mshindi kwanza kwa mwanaume ni milioni moja na nusu na kwa wanawake ni milioni moja.

  Pamoja na hayo wanamichezo hao wameaswa kufanya juhudi katika mchezo huu pia kutojaribu kutumia madawa ya kuongeza nguvu wakati wa michezo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HALMASHAURI YA KAHAMA YAASWA KUACHA KUCHUKUA TOZO ZISIZO NA UMUHIMU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top