728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 13, 2016

  FURSA MPYA KWA WAFANYABIASHARA TANZANIA.

  Wafanyabiashara wakubwa na wadogo nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za kujitangaza kibiashara mtandaoni ambazo hazina gharama zozote kwa mfanyabiashara. Hayo yameelezwa na Bwana Tushar Sharma kutoka kampuni ya Leo Leo inayotoa huduma hizo.

  Katika mahojiano maalumu na mtandao huu jijini Dar es Salaam, Bwana Tushar alisema ‘tumefungua mtandao mpya ambapo mfanyabiashara yoyote anaweza kujiunga na kutangaza biashara yake, bila gharama zozote. Pia na nafasi ya kipekee kwa watanzania kujipatia bidhaa mbalimbali zinazouzwa na wafanyabiashara hao’

  Kuhusu ukubwa wa biashara ambazo zinaruhusiwa katika mtandao huo, Bwana Tushar alisema ‘Hakuna kigezo cha ukubwa wa mtaji wala aina ya biashara, mtandao wetu wa www.leoleo.co.tz hauna ubaguzi wowote, unamruhusu mtu yoyote hata awe na biashara kubwa au ndogo kiasi gani, unajiunga na kutangaza biashara yako.’

  Hizi ni habari njema kwani, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa mtandao wa internet nchini Tanzania. Inakadiriwa kuwa kuna watumiaji wa Internet kiasi cha milioni kumi na moja nchini, hivyo hawa wote wana nafasi ya kufikiwa na biashar yako bila kulipia gharama zozote. 
  Mtandao huu umekuja wakati muafaka ambapo, kumekuwa na upungufu wa ajira nchini, hivyo ni fursa nzuri kwa vijana kujiari kwa kufanya biashara kupitia mtandao wa Leo Leo. Unaweza kutembelea mtandao huo hapa (hyperlink www.leoleo.co.tz) au kutazama kurasa zao za mitandao ya kijamii hapa Facebook (www.facebook.com/leoleotanzania), Instagram (www.instagram.com/leoleotanzania) au Twitter (www.twitter.com/leoleotanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: FURSA MPYA KWA WAFANYABIASHARA TANZANIA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top