728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 18, 2016

  BLESSING KUFAYA UCHANGIAJI WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WASIO NA UWEZO.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Tasisi ya Blessing.
   Mwanzilishi wa Taasisi ya Blessing, Blessing Mlanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa Taasisi ya Blessing, Zawadi Mlanga.
   Mwanzilishi wa Taasisi ya Blessing, Blessing Mlanga akionesha Tsheti amazo zitavaliwa siku ya 23 ambazo zitauzwa kwaajili ya kuchangi pamoja na kuongeza nguvu za kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao hawana nguo nzuri pamoja na wasio na viatu vya shule na mabegi ya shule. Kulia ni Meneja wa Taasisi ya Blessing, Zawadi Mlanga.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Mkakati wa  Rais Dk. John Pombe Magufuli  wa elimu bure unatekelezwa kwa vitendo katika kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu ,huku Taasisi ya Blessing  imekuja na mkakati wa kusaidia wanafunzi wasio na vifaa pamoja sare za shule.

  Taasisi hiyo inatarajia kufanya uchangishaji kwa ajili ya kupata vifaa pamoja na sare za shule kwa wanafunzi ili waweze kusoma bila changamoto vitu hivyo.

  Uchangiaji huo unatarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu katika ukumbi wa Nkurumah katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

  Meneja wa Taasisi hiyo, Blessing  Mlanga amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wanachangamoto ya vifaa na sare hivyo ikiwa watanzania tunaweza kuchangia sehemu hiyo na kuwa tumeunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli.

  Zawadi amesema kuwa yeye ni kijana wa kitanzania anayesoma Malaysia ameona kuna sehemu ambayo anaweza kuboresha katika upande wa vifaa pamoja na sare.

  Amesema kuwa mradi huo wa sare na vifaa utaanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Arusha na baada hapo wataendelea na mikoa mingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BLESSING KUFAYA UCHANGIAJI WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WASIO NA UWEZO. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top