728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, July 29, 2016

  Benki ya TIB Corporate yatoa msaada wa mabati 100 kwa shule za mkoa wa Songwe.

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akipokea msaada wa bando za bati kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege (wa pili kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Mkoa Mpya wa Songwe.Wa kwanza Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mbozi, Erik Ambakisye akifuatiwa na Mbunge jimbo la Vwawa Josephat Hasunga

  Benki ya TIB Corporate leo imetoa msaada wa mabati mia moja kwa mkoa wa Songwe ili kusaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na vyoo mkoani humo.

  Mkoa wa Songwe, ambao ni miongoni mwa mikoa mipya, itatumia mabati hayo katika shughulli za ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wilaya za Mbozi, Mamba, Ileje, Songwe na Tunduma.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TIB Corporate, Bwana Frank Nyabundege alisema msaada huo umelenga kuonyesha nia na jitihada za benki yake katika kusaidia kukuza elimu na pia kuunga mkono serikali katika jitihada zake za kuboresha elimu nchini.

  'Serikali pekee yake haiwezi kukuza sekta ya elimu hivyo basi ni muhimu tuisaidie serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuaanda mazingira mazuri kwa vijana wetu kujisomea’ alisema Nyabundege.

  Akitoa shukrani zake kwa benki ya TIB Corporate, Mkuu wa mkoa wa Songwe Mheshimiwa Chiku Gallawa alisema mchango huo ni muhimu katika kukuza na kuboresha sekta ya elimu ambayo ndio kichocheo cha ukuaji wa sekta ya uchumi na kijamii kwa taifa la kesho.

  ‘Tunaishukuru benki ya TIB Corporate kwa jitihada zake za kushirikiana na serikali katika kukuza sekta ya elimu kwani hakuna taifa linaloweza kuendelea bila kuwa na raia wasomi ' alisema Mheshimiwa Gallawa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Benki ya TIB Corporate yatoa msaada wa mabati 100 kwa shule za mkoa wa Songwe. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top