728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 28, 2016

  BALOZI WA CANADA NCHINI AAGANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO


  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja.
  Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. Balozi huyo alimtembelea Profesa Muhongo kwa ajili ya kumuaga mara baada ya muda wake kumalizika hapa nchini.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimweleza Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) mikakati ya Serikali katika uboreshaji wa sekta ya nishati nchini .
  Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo (kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (hawapo pichani)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BALOZI WA CANADA NCHINI AAGANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top