728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, July 29, 2016

  BABATI WATAKIWA KUJIUNG ANA CHF ILIYOBORESHWA

  MKUU wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amesema atawachukulia hatua kali viongozi wa ngazi ya Vijiji, Kata, na Tarafa za Wilaya ya Babati, watakaozembea zoezi la kuhamasisha kaya zijiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (ICHF).

  Dk Bendera aliyasema hayo mbele ya mkuu wa Wilaya hiyo Raymond Mushi, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Hamis Malinga, wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Goroa, alipotembelea kuhamasisha kaya kujiunga na mfuko huo.

  Hata hivyo, amewaagiza viongozi hao kuhakikisha hadi mwezi Desemba mwaka huu kaya 40,642 zinajiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (CHF) hivyo kufikia asilimia 50 ya kaya zilizopo kwenye wilaya hiyo. Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo ya Babati ina kaya 81,284 hivyo viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe hadi mwezi Desemba wawe wamefanikisha nusu ya kaya zijiunge na mfuko huo.

  “Suala la kupatiwa matibabu pindi mtu akiugua halina mjadala hivyo viongozi wa ngazi tofauti kwenye wilaya hii ya Babati, wanapaswa kufuatilia ili kaya hizo zijiunge na mfuko huo ambao una manufaa kwao,” alisema Dk Bendera. Alisema viongozi wote wa eneo hilo wanapaswa kuhakikisha jamii inajiunga na mfuko huo kwani ni ukombozi wao kwenye sekta ya afya na siku wakistaafu wananchi watawakumbuka kwa kusababisha mabadiliko ya huduma hizo.


  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Goroa Wilayani Babati, juu ya kaya zao kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF).

  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Goroa Wilayani Babati, juu ya kaya zao kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF).

  Wananchi wa Kata ya Duru Tarafa ya Goroa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakimsikilimza Mkuu wa Mkoa huo Dk Joel Bendera wakati wakiwaeleza umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Hamis Malimba akizungumza kwenye mkutano wa ndani juu ya mikakati yake ya kuhakikisha kaya za wilaya yake zinajiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF).
  Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Raymond Mushi akizungumza na viongozi wa Tarafa ya Goroa juu ya mikakati yake ya kuhakikisha jamii inajiunga na CHF iliyoboreshwa.
  Hata hivyo, Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani humo, Isaya Shekifu alisema mpango wa CHF ulioboreshwa utawawezesha kila kaya ya watu sita baba, mama na watoto wanne ambao hawajafikisha miaka 18 kupata matibabu kwa gharama ya sh30,000 katika mwaka mzima.

  Shekifu alisema bima ya afya ni muhimu kwa sababu siyo kila mtu anapopata ugonjwa ana uwezo wa kugharamia matibabu na nchi zilizoendelea zimefanikiwa kupunguza vifo visivyo na lazima kwa kuhakikisha watu wanajiunga na mfuko. Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Hamis Malinga akizungumza mbele ya Dk Bendera, alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa wananchi wa eneo hilo wanajiunga kwa wingi na mfuko huo.

  Malinga alisema kupitia timu waliyonayo kuanzia ngazi ya vijiji, kata na tarafa, watatimiza majukumu yao kwa kupeana mrejesho kila mwezi ili kutambua wamefikia hatua gani na wanatarajia hadi mwezi Desemba watafanikisha suala hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BABATI WATAKIWA KUJIUNG ANA CHF ILIYOBORESHWA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top