728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 13, 2016

  AZANIA BANK YATOA MADAWATI 75 KONDOA

  BENKI ya Azania Ltd imetoa madawati 75 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF) ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kila mwezi kutoa sehemu ya mapato kwa ajili ya kusaidia jamii.

  Akizungumza katika hafla ya utoaji wa madawati hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Azania, Nurdin Semnangwa, alisema: “Mwaka huu kwa kuitikia mwito wa kilio cha madawati kwa wanafunzi wetu wa shule za msingi na sekondari, benki ya Azania ilidhamiria kuhakikisha wanafunzi 1,200 wanapata madawati ya kukaa.”

  Aidha, Semnangwa aliongeza: “Leo tunatoa kiasi cha shilingi milioni sita kuweza kuondoa tatizo la kukaa chini wakati wa masomo ili yapatikane madawati 75…kwa watoto 225 wa wilaya za Kondoa na Chemba.”Semnangwa alisisitiza kwamba utoaji wa madawati utaendelea katika siku za usoni kwenye mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu, Songwe na Dar es Salaam kwani walishafanya Kilimanjaro.

  “Madhumuni yetu ni kuendelea kujitolea sehemu ya faida kwa jamii ya Watanzania wakati wowote,” alisisitiza Mnangwa.Kwa upande wake Mwenyekiti wa KDF, Balozi mstaafu Cyprian Majengo alisema: “Tunaishukuru Benki ya Azania, asasi hii imekuwa ikishughulika na wilaya zote mbili (Kondoa na Chemba) kwa kuzingatia hilo msaada huu utapelekwa kwenye maeneo hayo.”

  “Tangu kusajiliwa kwake (2002) asasi imesaidia mambo mengi katika kuleta maendeleo ya wilaya zote mbili…ujenzi wa madarasa kwa kutoa vifaa vya ujenzi, kutafuta bei nzuri ya zao la mbaazi, alizeti na ufuta, kupeleka walimu wa muda kutoka vyuo vikuu wakati wa likizo katika shule za sekondari,” alisema Majengo.

  Hata hivyo alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kwa wingi kuitazama jamii hususan kwa changamoto ya sasa ya ukosefu wa madawati katika shule za msingi na sekondari.

  Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (wa pili kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo.
  Kukabidhi mfano wa hundi.

  Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa akizungumza katika hafl fupi ya kukabidhi hundi ya shs. milioni 6 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF) jijini Dar es Salaam itakayosaidia ununuaji wa madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba mkoani Dodoma. (Picha na Francis Dande)
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo kwa ajili ya kununulia madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam .
  Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (katikati) akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya Shs milioni 6 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF).
  Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (katikati), akimkabidhi hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo kwa ajili ya kununulia madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mweka Hazina wa KDF, Abdilay Mvula.
  Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo kwa ajili ya kununulia madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: AZANIA BANK YATOA MADAWATI 75 KONDOA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top