Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania na kampuni ya StarTimes walipotembelea studio za StarMedia zilizopo mjini Beijing nchini China leo kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na studio hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa akifuatiwa na Erick Xue, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang akifuatiwa na Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya nchi za nje wa StarTimes William Lan.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akifanya mahojiano na mtangazaji wa StarTimes ambaye ni Mtanzania David (kushoto) wakati alipotembelea studio hizo leo zilizopo mjini Beijing nchini China kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na studio hizo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) na Rais wa kampuni ya kimataifa ya StarTimes Pang Xinxing (kushoto). Mhe. Naibu Waziri alitembelea studio za StarTimes zilizopo mjini Beijing nchini China leo kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na studio hizo.
Picha na mpigapicha wetu
No comments:
Post a Comment