JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TASMA KUNOGESHA TAMASHA LA ‘KANDANDA DAY’ OKTOBA 17 MWAKA HUU

Share This
CHAMAcha Madaktari wa michezo Tanzania (TASMA) kinatarajia kunogesha tamasha la ‘Kandanda day’ kwa kufanya kliniki siku ya Oktoba 17,mwaka huu katika Viwanja vya TCC Chang’ombe,jijini Dar es Salaam.

Msemaji Mkuu wa tamasha hilo,Mohamed Mkangara,alisema kwamba TASMA kwa kushirikiana na kamati ya kandanda Day wameamua kufanya kliniki hiyo ya wazi ili kuwapa fursa wadau wa michezo kupata mafunzo na kupima afya zao.

“Kamati ya Kandanda day,imeona kuna haja ya kushirikiana na ndugu zetu wa TASMA,ili kutoa elimu ya afya,kwa wadau wa michezo nchini ambao watapata fursa ya kupima afya zao bure,na baadaye watapata burudani ya kuangalia burudani ya mechi kati ya timu Dizo One na timu Ismail,”alisema 

Mkangara na kuongeza:
“Kikubwa tunawashukuru sana TASMA kwa kuitikia mwito wetu wa kushirikiana nasi katika siku hiyo muhimu, hususan kwa wapenda soka nchini,halikadhalika wadhamini wetu kampuni ya Bin Slum Tyres kwa kutusaidia zoezi hili la kliniki.”

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa TASMA, Dk. Nassoro Matuzya,alisema kwamba maandalizi yote kuhusiana na clinic hiyo yanaendelea vizuri na ametoa mwito kwa wadau wa michezo nchini hususan wa soka,kujumuika kwa wingi katika viwanja hivyo.

“Kwa upande wetu tunawashukuru kamati ya Kandanda,kutujumuisha katika tamasha hilo kutoa elimu pamoja na kutoa huduma ya upimaji afya kwa Watanzania wanamichezo na wadau wa michezo nchini,kwa hiyo tunapenda kuwakaribisha wadau wajitokeze kwa wingi katika siku hiyo,”alisema Matuzya.

Tamasha la mwaka huu mbali na kiliniki pia kutakuwa na shughuli mbalimbali za soka na burudani zikiendelea,ambazo zimepata kuongezewa nguvu na udhamini kutoka kampuni ya matairi ya Binslum.SBS kupitia kinywaji chake cha Pepsi.Michuzi Media group,Blogu ya Saleh Jembe.kampuni ya kutoa mikopo ya Bayport pamoja na kampuni ya kuchapisha matangazo ya SDS.

Kiliniki itaanza asubuhi saa mbili kamili kwa wadau wa michezo kupata mafunzo kutoka kwa madaktari wa TASMA na kufuatiwa na michezo ya soka na burudani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad