JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHINDANO LA SERENGETI MASTA LAWASHA MOTO ULAYA ULAYA BAR YA MANZESE

Share This
Mshereheshaji wa shindano la Serengeti Premium Lager liliopewa jina la “Serengeti Masta” Razani Kapalatu akiwa pamoja na mabalozi wa bia ya Serengeti premium Lager ambao kwa pamoja walitoa maelezo kwa wateja wa bia hiyo waliofika kushiriki katika shindano la kumtafuta Serengeti Masta ndani ya baa ya Ulaya Ulaya iliyopo Manzese jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Shindano hilo limedumu jijini Dar na mikoani kwa takriban muda wa miezi miwili sasa na kuweza kuzifikia baa mbalimbali ambapo zawadi mbalimbali kama fedha taslim, fulana na bia za bure zimekuwa zikitolewa katika kuwahamasisha wateja wa bia hiyo kuendelea kuwa pamoja.
Mshereheshaji wa shindano la Serengeti Masta Razani Kapalatu akitoa zawadi ya fulana kwa mkazi wa Manzese na mpenzi wa bia ya Serengeti Premium Lager Rodgers Robert wakati wa promosheni ya kumtafuta Serengeti Masta iliyofanyika katika baa ya Ulaya Ulaya ya Manzese jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya bia ya Serengeti Premium Lager imezifikia baa zaidi ya mia tano kwa mikoa minne ambayo ni Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya na kufanikiwa kutoa elimu juu ya bia hiyo na ubora wake.
Mkazi wa Magomeni jijini Dar es salaam Sam Stima akifurahia zawadi yake ya fulana kutoka kwa balozi wa bia ya Serengeti Premium Lager Razani Kapalatu wakati wa promosheni ya Serengeti Masta iliyofanyika katika baa ya Ulaya Ulaya iliyopo Manzese jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya bia ya Serengeti Premium Lager imefanikiwa kuwafikia wateja na wahudumu wa baa mbalimbali katika kipindi cha miezi miwili ikitoa zawadi ya fedha taslim na elimu kuhusiana na ubora wa bia yake.
 Mshereheshaji wa shindano la Serengeti Masta Razani Kapalatu( akionyesha kiasi cha Tsh. 50,000/= alichomkabidhi mshindi wa shindano la Serengeti Masta ambaye aliitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager wakati wa promosheni hiyo iliyofanyika katika baa ya Ulaya Ulaya iliyopo Manzese jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni mteja aliyeibuka “Serengeti Masta” wa baa hiyo ambaye alifahamika kwa jina la Doris Frances.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad