JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


AIRTEL YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

Share This
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel , Sunil Colaso (wakwanza kulia), Mkurugenzi
wa Kitengo cha huduma kwa wateja, Adrian Lyamba(katika) na wafanyakazi 
wa Airtel kwa pamoja wakikata keki kuzindua wiki ya huduma kwa wateja 
duniani inayoanza rasmi tarehe 5 octoba 2015. Halfa hiyo ya uzinduzi 
ilifanyika katika makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kitengo cha huduma kwa wateja, Airtel Tanzania, Bwn  Deo Hugo akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika katika ofisi za Airtel Makao makuu Moroco, wakifatilia kwa makini ni baadhi ya wafanyakazi waliohudhuria uzinduzi huo
 Meneja huduma katika kitengo cha huduma kwa wateja, Zakia Omary
akionge wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja, pichani
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso (kulia) akiwa na wafanyakazi wa
vitengo mbalimbali.
 Wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wakiwa katika picha ya
pamoja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika
katika makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso akiongea na wafanyakazi
(pichani hawapo) wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja

KAMPUNI Airtel Tanzania imezindua.
maadhimisho ya  wiki ya huduma kwa wateja, na ujumbe wa mwaka huu
"Mimi ni Airtel ninajivunia kukuhudumia".I am Airtel proud to serve
you" . Kuadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja, Wakurugenzi, Mameneja na mabalozi wa Airtel watakuwepo katika maduka yote ya Airtel kuhakikisha wanakutana na wateja na kusikiliza maoni yao.



Airtel ambayo ina wateja zaidi ya milioni 10 nchini nzima, imechukua
fulsa ya kushukuru wateja wake katika wiki hii ya huduma kwa wateja
kwa kuwa waaminifu, wavumilivu na kwa kuchagua mtandao wa Airtel
kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa na marafiki popote pale walipo
hapa nchini. Airtel inaahidi kuendelea kuwekeza kwenye mtandao na
kujinajipanga kuendelea kuwapa huduma bora na za kisasa ikiwemo
intanet yenye kasi zaidi, huduma ya Airtel Money na mawasiliano bora
kwa gharama nafuu zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi, Adriana
Lyamba, alisema katika taarifa yake kuwa, "wiki hii ya huduma kwa
wateja itaambatana na mambo mengi yatakayofanywa na wafanyakazi wa
Airtel kwa lengo la kumfaidisha mteja. Tutakutana na kuwasiliana na
wateja wote wa ndani na nje kwa lengo la kuendelea kutoa  huduma bora
na yenye viwango vya hali ya juu.

 Sisi Airtel tunaamini wateja wetu
ndio sehemu kuu ya mafanikio yetu. Kutoa huduma inayokithi mahitaji ya
wateja wetu ndio lengo letu kubwa katika biashara na dhamira yetu ya
kutoa huduma yenye uzoefu tofauti wakati wote na kwa wateja wetu wote
nchi nzima" 

"Katika wiki hii ya huduma kwa wateja, tunawapelekea wateja wetu


huduma popote pale walipo, kusikiliza maoni yao  na vile vile
kuwashukuru kwa uaminifu wao na kuweza kuwa nasi katika kipindi chote
walichokuwa nasi " aliongeza Lyamba.

Kilele cha wiki ya huduma ya wateja kitakuwa mwishoni mwa wiki hii,
itakayohitimishwa na sherehe ya kuwatunuku wafanyakazi bora wa kitengo
cha Airtel huduma kwa wateja kwa kukabidhiwa zawadi kwa kutoa huduma
bora kwa wateja wa Airtel , kuoonyesha taaluma na kujituma na kazi zao

katika kipindi kizima cha mwaka huu .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad