JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Share This
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
 
        “PRESS RELEASE” TAREHE 03.09.2015.

·         MTU MMOJA AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYA YA MBARALI.

·         MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYA YA MBOZI.

·         WATU SITA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA OPERESHENI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BOKA KASULA (50) MKAZI WA SONYANGA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI ALP 3965 AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA WADACHOVU ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ERNEST CLEMENCE (42) MKAZI WA ILOMBA IKITOKEA DSM KUELEKEA MALAWI.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA SONYANGA, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA IGURUSI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA. UPELELEZI UNAENDELEA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
 MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THADEO MWASHILANGA (21) MKAZI WA ICHENJEZYA WILAYA YA MBOZI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILOLO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI NA DEREVA ALIKIMBIA NA GARI BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

TAARIFA ZA MISAKO:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AIDAN JOHN (32) MKAZI WA UYOLE-MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 25.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO ENEO LA MATENKI, KATA YA NJISI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA AITWAYE MWINUKA NGONYA (30) MKAZI WA MATENKI  AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA RIDDER BOKSI 08 NA CHARGER BOKSI 2.

AIDHA KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA WILAYANI CHUNYA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI [B], KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA GEORGE SAWELA (44) MKAZI WA MATUNDASI NA GILBERT SILWANI (43) MKAZI WA MATUNDASI WAKIWA NA MILIPUKO BARUTI 136 PINI ZA MILIPUKO 35, COTEX MITA 70 NA DOTNETOR 2 BILA KIBALI.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA ZINAENDELEA.

Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad