JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


DK.SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Share This
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi sana tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo  chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho. Leo ameibuka na kusema  ya moyoni kuwa amejivua uanachama  rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuu wa Chama hicho na kuachana  kabisa na siasa  kutokana na mambo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya chama chake hayakumridhisha na hakukubaliana nayo.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndio maana ameamua kuachana na siasa  rasmi hii leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.

Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk.  Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad