JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MUHIMBILI 1988 WAIKUMBUKA SHULE YAO.

Share This
Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, akikata utepe ili kufungua Ofisi ya walimu wa shule ya msingi Muhimbili, iliyokarabatiwa na kuweka viti 29 na meza 8 na wanafuzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo Mwaka 1988, pamoja na kiti na meza ya kisasa katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo katika hafra fupi iliyoandaliwa na wanafunzi hao ikiwa imehudhuliwa na walimu wa shule hiyo wa tangu mwaka 1978.
 Walimu wa Shule ya Msingi Muhimbili wakifurahia kupewa viti vipya pamoja na meza na wanafunzi wao waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo, wamekabidhiwa Samani hizo leo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muhimbili, Dafrosa Assenga akipeana mkono na Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, mara baada ya kukabidhiwa kiti na meza Mpya kutoka kwa wanafunzi waliohitimu katika shule hiyo Mwaka 1988, ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza elimu katika shule hiyo.Kutoka kulia ni Mhitimu wa shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988 na Mkurugenzi wa Galaxy Cargo, Jonatha Kasesele, Mwenyekiti wa wahitimu 1988  shule ya msingi muhimbili,Usia Nkoma
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy na  Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Muhimbili, George Ntevi.
Mwalimu wa shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1986 hadi sasa, Marry Massawe akiwashukuru wanafunzi waliosoma shule hiyo kwa kuikumbuka shule yao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Muhimmbili mwaka huu wakiwa wamehudhulia hafra fupi ya wahitimu wa shule hiyo mwaka 1988 leo jijini Dra es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad