JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BUNGE LA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI MKOANI MANYARA WAFANIKIWA KUWARUDISHA WATOTO WA MITAANI SHULE

Share This

Abdallah Waziri - ambaye ni mmoja wa watoto wa mitaani aliyerudishwa shule kwenye kikao cha leo.
Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake katika kikao  cha bunge katika shule ya oysterbay mkoani manyara.
Mbunge Nasri Selemani akifuatilia hoja kwa makini wakati kikao cha bunge la watoto likiendelea katika shule ya oysterbay mkoani manyara.


 Mbunge Nasri Selemani ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa nyumbani na sasa kwa jitihada za bunge amerudishwa shuleni,,akichangia hoja.
Mtangazaji wa Kipindi cha Tafakari Time Benedicta Mrema akizungumza na Abdallah Waziri na kumkabidhi mchango wa shilingi 57,800 aliochangiwa kwa ajili ya kumuwezesha mahitaji ya shule.
Raisi wa Bunge la watoto Oysterbay, Manyara - Sarah David akitoa hotuba ya ufunguzi wa bunge la watoto katika shule ya oysterbay mkoani manyara.
Wabumbe wa Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.
Wajumbe a Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.
Waliosimama, Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
MTANDAO wa  Marafiki wa Elimu Babati (BADENET) ulianzishwa mwaka 2012 chini ya uongozi wa Asia Mtibua, mtandao huu ulianzishwa kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za elimu pamoja na kuanzisha kituo cha kupashana habari.

Moja ya mafanikio ya BADENET ni kuanzishwa kwa Bunge la Watoto katika shule ya msingi Osterbay mkoani Manyara, bunge hili lilianzishwa kwa lengo la kuwaleta pamoja watoto waliopo shuleni na ambao wapo nje ya shule ili waweze kujadili masuala ya elimu ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kuweza kusikilizwa wao kama watoto. 

Bunge hili la watoto linajumuisha wajumbe 43 (26 wasichana na 17 wavulana) na hukutana mara 1 kwa kila mwezi. Mpaka sasa jumla ya watoto wa mitaani 19 wamerudishwa shuleni na wanasoma, wapo wanaoingia asubuhi na wengine mchana.

Leo hii Bunge la watoto Oysterbay mkoani Manyara limekutana kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili  watoto wa mitaani “Chokoraa” ili kuzungumza namna ambavyo watawawezesha  watoto hao kupata fursa ya elimu kama watoto wengine waliopo shuleni. 

Katika kikao cha leo bunge limefanikiwa kumrudisha shuleni mtoto Abdala Waziri ambapo alichangiwa na wabunge, marafiki wa elimu na walimu jumla ya shilingi 57,800 ili zimuwezeshe kununua mahitaji muhimu ya shule.

Mkakati wa bunge la watoto katika shule ya msingi Osterbay ni kuhakikisha kuwa kila mbunge anamrudisha shuleni mtoto yoyote ambaye yuko mtaani na kuhakikisha wanafurahia fursa ya kupata elimu ambayo ni haki yao ya msingi.
Timu ya Tafakari Time, kipindi kinachorushwa kila siku ya alhamisi kupitia ITV ilishiriki kikao cha leo kwa lengo la kujifunza uendeshwaji wa shughuli za bunge hili la watoto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad