728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, May 21, 2013

  PROF JAY KAJIUNGA NA CHADEMA ?


  Pichani ni Prof Jay akionesha kadi yake baada ya kukabidhiwa kadi hiyo ya CHADEMA akiwa sambamba na Mh.Joseph Mbilinyi. Professa Jay ametangaza rasmi kuwa mwanachana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria bunge la bajeti mapema jana akiwa sambamba na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Mwanadada Lady Jay Dee. Kwa mujibu wa picha ambazo amekuwa akizisambaza kwenye mitandao ya kijamii msanii huyo alionekana akiwa na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi huku akiwa amekamatia kadi ya chama hicho kama aonekavyo pichani.
  Pichani kati ni Msanii maarufu na mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Haule almaarufu kwa jina la kisanii kama Pro.Jay akiwa kwenye mchakato wa kujiunga na chama cha CHADEMA,mjini Dodoma,kwa taarifa zinaeleza kuwa Prof Jay  amekwishajiunga na chama hicho akiwa tayari ni mwanachama halali,kulia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA),Mh.John Mnyika na kushoto ni Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini (CHADEMA),Mh.Joseph Mbilinyi.Aidha inaelezwa kuwa Professa Jay amekabidhiwa kadi hiyo na Mbunge wa Mbeya mjini 'Joseph Mbilinyi' a.k.a Sugu.kujiunga kwa msanii huyo katika chama hicho kuna uwezekano akagombea ubunge 2015.!!!!!
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: PROF JAY KAJIUNGA NA CHADEMA ? Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top