Tuesday, July 31, 2012

dkt asha-rose migiro akutana na mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji mstaafu joseph Warioba

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt.Asha-Rose Migiro (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji  Mstaafu Joseph Warioba wakati Dkt. Migiro alipotembelea ofisi zaTume jijini Dar es Salaam leo (Julai 31, 2012). (Picha na Ismail Ngayonga).

BEACH PLOT IN BUKOBA----FOR SALEBeach plot , ufukwe wa Ziwa Victoria kaskazini mashariki mwa mji wa
Bukoba. Kilometa 4 kutoka Bukoba airport.
Plot ina Title deed na ina ukubwa wa Mita za mraba 15408.

email kyatwap@yahoo.com 
au spika2003@gmail.com  
au pkyatwa@gmail.com

0658499188 au 0756499188

au kwa namba hizi              +26773309420 begin_of_the_skype_highlighting            +26773309420      end_of_the_skype_highlighting      
 au             +26772870064 begin_of_the_skype_highlighting            +26772870064      end_of_the_skype_highlighting      
 au             +26774101642 begin_of_the_skype_highlighting            +26774101642      end_of_the_skype_highlighting      .

samahani:  madalali hawana nafasi.

TAHADHARI YA UGONJWA WA EBOLA

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kuwepo ugonjwa wa Ebola ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda. Maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo ni Kanda ya Magharibi ya nchi hiyo ambapo takriban watu 20 wamepata maambukizo na kati yao, 14 wamepoteza maisha. Hadi kufikia tarehe 29 Julai 2012 kuna wagonjwa wawili waliolazwa na hali zao zinazidi kuimarika.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale waliopo katika mikoa ambayo inapakana na nchi jirani ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma na Rukwa).

Chanzo na dalili za ugonjwa wa Ebola

Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini.

Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi.
Kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa njia zifuatazo:

o Kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo

o Kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu.

o Kugusa wanyama walioambukizwa (mizoga na wanyama wazima) kama vile sokwe na swala wa msitu.

Tiba na chanjo ya Ebola
Mpaka sasa ugonjwa wa Ebola hauna tiba wala chanjo.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu nchini:

o Kutoa taarifa ya tahadhari kuhusu ugonjwa huu kupitia kwa waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya. Aidha, taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),  “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa sekta ya afya wa namna ya kuchukua sampuli na vipeperushi vinavyoelezea ugonjwa huu.     

o Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa wataalam wa Afya katika Mikoa, Wilaya na Maeneo ya mipaka. Aidha, watalaam wa Afya pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu, ili endapo ugonjwa huo ukitokea uweze kutolewa taarifa mapema.

o Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya. 

Wito
Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa hapa nchini. Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu, mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.

Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
31/7/2012.

WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA TOVUTI YA SEKRETARIETI YA AJIRA

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amewataka wahitimu na wale wote wenye kutafuta fursa za ajira Serikalini kujijengea utamaduni wa kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira mara kwa mara kwani kila nafasi za ajira zinapojitokeza huwekwa katika tovuti hiyo ili kutoa fursa kwa wadau walioko nje na ndani ya nchi kuweza kuziona kwa urahisi.

Amesema hayo leo, wakati akiongea na mwandishi wa habari ofisini kwake aliyetaka kujua fursa za ajira zilizoko na taratibu za mchakato wa ajira tangu kutolewa kwa tangazo hadi kupangiwa kituo cha kazi.

Daudi amesema, kwa mfano mwananchi yeyote akitembelea katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira hivi sasa ataona tangazo la kuitwa kazini kwa waombaji kazi waliofaulu katika usaili uliofanyika mwezi Juni, 2012 ambao wanatakiwa kuripoti kwa Waajiri; Wakala wa Vipimo, pamoja na kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mbali na hilo, pia watakuta tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo kulingana na nafasi walizokuwa wameomba kama zilivyokuwa zimetangazwa kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Chuo cha Mipango Dodoma, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na taasisi nyinginezo.

Aliongeza kuwa katika Tovuti hiyo watakuta pia tangazo la nafasi za kazi 194 zikiwemo nafasi za Wakurugenzi, Wakufunzi Waandamizi wa Vyuo, Wakufunzi Wasaidizi, Wahandisi, Mafundi Sanifu, Wakaguzi wa ndani wa hesabu, Makatibu Mahsusi, Walinzi, Wapishi na kada nyinginezo.

Aidha, amesisitiza ni muhimu kwa waombaji kuzingatia masharti ya tangazo pindi wanapotuma maombi yao kwa njia ya posta ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata fursa ya ajira serikalini maana mchakato wa ajira hufuata Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu .Katibu wa Sekretarieti ya Ajira alimaliza mahojiano yake kwa kuitaja tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuwa ni www.ajira.go.tz kwa wale wasioifahamu ili waweze kuifahamu.

NA: Riziki Abraham
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
31/07/2012.

Mfalme Siboka kuzindua albamu yake Msimu wa Nanenane kanda ya ziwa.

MFALME wa nyimbo za asili nchini, Costa Siboka, anatarajia kuzindua albam yake ya ‘Nderule’ kwenye  msimu wa sherehe za Nanenane mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa udhamini wa kinywaji cha Konyagi.


Akizungumza jijini Dar es Salaam,  Siboka alisema kua  amejiandaa vya kutosha kwa udhamini huo mkubwa wa kapuni ya Tanzania Distilleries Limited watengenezaji wa Konyagi,  ambapo  aliwashukuru na kuwaadi mashabiki wake kujitokeza kwa wingi Mkoani Shinyanga,  Agost 8, siku ya  Nanenane na baada ya hapo ataendelea mikoa mingine ya Kanda hiyo ya Ziwa.  “Bendi yangu  imejiandaa vya kutosha  kwa uwezeshwaji wa bia ya Konyagi, tutapiga shoo sambamba na uzinduzi wetu  wa Albam ya pili ya  ‘Nderule’ hivyo  tunaomba kujitokeza kwa wingi wakazi wa Shinyanga hiyo siku ya Nanenane” alisema Siboka.


Siboka  aliongeza  kua, mbali na  uzinduzi wa Albamu hiyo  ya pili, pia bendi yake itafanya kweli kwa mashaibiki wake wake kwa kuonesha vitu vipya na kusuuza roho zao kutoka kwa wanenguaji wake wakiwemo wa zamani na wapya, ambao ni pamoja na Halima Ndembendembe, Fadhira Mitikisiko, Salama Kadogoo na Queen Mwanasesere, ambao  wote walipata  mafunzo kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo.


Pia alizitaja nyimbo  ziizo kwenye albam yake hiyo  yenye nyimbo sita, kua ni pamoja na ‘Butereakaila’, Busoma basi’, ‘Omwana  kalikwela’  na zingine nyingi. Aidha, alisema mashabiki wake kwenye ziara hiyo watabahatika na kuzisikia na nyimbo zake zinazotamba za albam yake ya kwanza ya ‘Niwewange’ ambapo nazo atazipiga kwa mashabiki wake, aliwataja wadhamini wengine kua ni Balimi Extra, Zizou fashion,Sisi entertainment, CXC Africa, Precision air na wengine.

WASANII KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU

Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agizo kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.

Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.

Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.

Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.

Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.

Asante.

tafadhali wadau mpigieni kura mtani wetu prezoo.


Kindly vote him via SMS by writting PREZZO and send your vote to any of the below numbers based on the Country you are:- Please let all your family and friends around Africa Continent Vote for him.
NB:- SMS Votes are the votes which count and not twitter or face book.
ANGOLA - 43333
BOTSWANA - 16626
GHANA - 1474
LIBERIA - 2626
MALAWI - 15626
SI ERA-LEON - 2626
SOUTH AFRICA - 33929
ZAMBIA - 4333 / 15626
ZIMBABWE - 33334 / 15626
NIGERIA – 34350
UGANDA - 7626
KENYA -5626
TANZANIA – 15726
UGANDA - 7626
REST OF AFRICA - 2783142100414
We family of JACKSON MAKINI NGECHU … PREZOO we thank you in advance for your contribution.

WASANII TUNADHULUMIWA KWA KUKOSA UELEWA – MZEE JENGUA.

Mohamed Fungafunga

Mzee Jengua mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MSANII mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Mohamed Fungafunga ‘Mzee Jengua’ amesema kuwa wasanii wengi wamejikuta wakidhulumiwa au kupata malipo madogo kutokana na kazi ya uigizaji kutokana na kuwa na uelewa mdogo katika kuingia mikataba na baadhi ya watayarishaji wa filamu hapa nchini, Mzee Jengua akiongea na Mwanaspoti amesema baada ya kuligundua hilo yeye ameamua kumtafuta meneja wake ambaye atakuwa akipatana na kufuatilia kila kitu na kumweleza aigize katika filamu husika kama inamlipa kutokana na ushauri wa meneja wake.
Mohamed Funga funga
Mzee Jengua akiwa kazini.
“Wasanii wengi tuna matatizo katika uelewa, kutokana na hilo tunajikuta tukifanya kazi nyingi kwa ujira mdogo ambao kupiga hatua inakuwa kazi kuna baadhi ya waandaaji akitaka kukudhulumu au tuseme kukubaisha anakuletea mkataba labda umeandikwa kwa lugha ya kigeni na hakupi nafasi hata ya kwenda kujiuliza kwa mwanasheria au mtu mwenye uelewa na utaalamu wa mambo ya mikataba, ukiangalia na wewe unahitaji hiyo fedha basi unaingia mkenge,”anasema Mzee Jengua.
Katika kukabiliana na hali hiyo msanii huyo ameamua kuingia mkataba na meneja wa kusimamia kazi zake zote kwa mantiki hiyo mtayarishaji yoyote atawasiliana na meneja wake ili kuepuka matatizo na usumbufu ambao unaweza kutokea katika utendeji wa kazi hizo, Mzee Jengue ni moja kati ya wasanii wakongwe waliotamba sana katika michezo ya maigizo siku za nyuma iliyokuwa ikirushwa katika kituo cha Televisheni cha ITV akiwa na kundi la Kidedea.Habari zaidi kuhusiana na tasnia ya filamu na wasanii Bofya Hapa.

SCF conducts tailor made training for Sunflower oil and Dairy Processing SMEs in Tanzania to build internal competences


Small and Medium Enterprises Competitiveness Facility (SCF)’s Business Manager Michael Bulemo speaks to entrepreneurs in Dairy and Sunflower oil processing industries during the launch of a five-days tailor made training of food processing for SMEs Chief Executive Officers (CEOs) and their staff to build their capacity for both domestic and international competitiveness. The training is going on at Top Life hotel in Morogoro. Left is Head of Department of Agricultural Economics and Agribusiness (SUA – DAEA) Dr. Damas Philips and right is Lecturer Department of Agricultural Economics and Agribusiness (SUA Morogoro) Akyoo Meshack.
======  =======  ========  ======

SCF conducts tailor made training for Sunflower oil and Dairy Processing SMEs in Tanzania to build internal competences.

By Our Correspondent, Morogoro

Small and Medium Enterprises Competitiveness Facility (SCF) yesterday launched a tailor made training of food processing for SMEs Chief Executive Officers (CEOs) and their staff to build their capacity for both domestic and international competitiveness.  

Speaking shortly before officiating the training, SCF’s Business Manager Michael Bulemo said the training which involves SMEs in Dairy and Sunflower oil processing industries, will equip them with business management skills that can assist them to operate competitively in terms of producing quality products at reasonable cost with best marketing strategies.

He said the training will help them to improve their company’s internal management competencies, strengthen sourcing and distribution channels and also will introduce the basics of quality and food safety standards requirements by niche domestic and international markets.

A five day training which is held in Morogoro at Top Life Hotel is  being conducted by Sokoine University of Agriculture- Department of Agricultural Economics and Agribusiness (SUA – DAEA) under the auspices of (Sokoine University of Agriculture – Bureau of Agricultural Consultancies and Advisory Services (SUA BACAS).

Mr. Bulemo said this training will help SCF’s intention to address internal competencies gaps amongst food processing SMEs in Tanzania. Meanwhile, Head of Department of Agricultural Economics and Agribusiness (SUA – DAEA) Dr. Damas Philips said these gaps were identified by SCF in her mapping study that covered 100 registered food processing SMEs in Tanzania, its regular business mentoring visits to SMEs and through its value chain validation studies conducted in November 2011 and validated by stakeholders workshops in December 2011. 

Dr Philips said amongst the gaps in internal skills and competences identified included identification of market opportunities, whereby most SMEs are able to sell their products, but their volumes are small and prices are not very competitive due to high production costs.

“Adoption of appropriate market positioning, whereby most SMEs serve ‘all’ and by doing so, they lose focus and overstretch their resources, consequently their customers become unsatisfied by the products.

“Many SMEs in Tanzania have informal plans to bring their products in the market place, they do not put their operational and marketing plans on paper and they don’t work consistently towards achieving the planned goals. Many find it costly to formalise/document their strategy and engaging experts to assist in development of a bankable business plan,” said Dr. Philips.

On the other hand, Mr. Bulemo mentioned that the training would equip participants with the following skills; financial management skills, marketing, inventory management, cost structure, working capital planning, supply chain alignment, and quality and safety standards issues.

He also mentioned that SCF had introduced a Point of Sales (POS) database which was now available for food processors in the country at a cost of USD 100, to help them have easy access to crucial market information that will assist them access potential new markets and to increase their sales volumes.  

Monday, July 30, 2012

kumbukumbu-Jackson Mandan 30.10.2012

 JACKSON A. MANDAN (GOA)
30.10.1972 – 30.07.2008
 NI MIAKA 4 SASA TOKA ULIPOTUTOKA HAPA DUNIANI KAKA YETU MPEDWA. UNAKUMBUKWA SANA NA MAMA YAKO, BABA YAKO, MKE WAKO, WATOTO WAKO, WADOGO ZAKO. SISI TULIKUPENDA LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI AKAAMUA KUKUITA KATIKA MAKAO YA MILELE.
TUNAKUKUMBUKA SANA KAKA YETU MPENDWA.
BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA JINA LA BWANA LIBALIKIWE

RAIS KIKWETE AFUTURISHA MKOANI LINDI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi na waumini wengine wa Mkoa wa Lindi aliowakaribisha katika futari Ikulu ndogo ya Mkoani Lindi leo Julai 30, 2012.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wachungaji waliokuwa miongoni mwa wageni waalikwa
 Kadhi wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Shekhe Mkuu wa Mkoa Mohamed Saidi Mushangani akitoa neno la shukurani baada ya futari
 Mkuu wa Mkoa a Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akishiriki katika futari hiyo pamoja na waalikwa wengine
 Waalikwa wakipakua futari
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru waalikwa kwa kuhudhuria katika hafla ya futari aliyoandaa
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wageni waalikwa baada ya kufuturu

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi (kushoto) na Mkuu wa Idara ya  Uhamiaji ya mkoa waliokuwa miongoni mwa wageni waalikwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wageni wake baada ya futari.Picha na IKULU.

VOLUNTEERING TRAINING OPPORTUNITIES " NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI "

RafikiElimu   Foundation    kupitia  mradi  wake     EUV   Project   "  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Vijijini "  inatangaza  nafasi  za  mafunzo   ya  ualimu  wa  ujasiriamali    kwa  watanzania  wenye  sifa  zifuatazo :                               

     SIFA ZA MWOMBAJI 
1. Umri  miaka  kumi  na  nane  hadi  thelathini  na  tano.
2. Elimu  kuanzia  kidato  cha  nne  , sita  na  kuendelea.
3. Awe   raia  wa  Tanzania
4. Awe  tayari  kufanya   kazi  kama  mwalimu  wa  ujasiriamali   vijijini  katika  wilaya  yoyote  ya  Tanzania  bara  atakayo  pangiwa  na  asasi.

Mafunzo   Yatakayo Tolewa

Kwa  watakao  pata  nafasi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  wata  jifunza  mambo  yafuatayo:

i.   Utengenezaji  wa  sabuni.
ii. Utengenezaji  wa    mishumaa.
iii. Utengenezaji  wa   chaki.
iv.  Utengenezaji  wa  viatu  vya  ngozi.
v.  Usindikaji  wa  vyakula  na  matunda.
vi. Uongozi  wa  biashara

        Muda  Wa  Mafunzo:

Mafunzo  haya  yatatolewa  kwa  muda  wa  mwezi  mmoja  kuanzia   tarehe   01  Septemba  2012  hadi  tarehe  31  Septemba  2012.

ADA  YA MAFUNZO :  Ada  ya  mafunzo  ni  shilingi  Elfu  Ishirini  na  Tano  Tu (  Tshs  25,000/=)

 MALIPO  YA  ADA  YA  MAFUNZO :   Malipo  ya  ada  ya  mafunzo  yafanyike  kupitia

  Account  Number :  0152395997900  , CRDB  BANK
 Account  Name  :  RafikiElimu   Foundation

DHUMUNI  LA  MAFUNZO  :  

 Dhumuni  la  mafunzo  ni  kuwajengea  washiriki   uwezo  wa  kutoa  mafunzo  ya  ujasiriamali  kwa  wajasiriamali  wadogo  wadogo  waliopo  maeneo  ya  vijijini.

                         MUDA  WA  MAFUNZO
Mafunzo   yataanza  rasmi  tarehe   3  Septemba  2012  , na  yatafanyika  katika  miji  ya
  Dar  Es  salaam,   Arusha , Mwanza, Mbeya,  Dodoma,  Moshi  na  Tanga.
Mafunzo  yatakuwa  ni  kwa  nadharia  na  vitendo

                                      WALENGWA  WA  MAFUNZO  :
Walengwa  wa  mafunzo  ni    vijana  walio  hitimu  kidato  cha  nne, cha  sita  na  kuendelea  ambao  wanapenda  kufanya  kazi  kama  volunteers  katika  mradi   wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Vijijini  na  ambao  wapo  tayari  kutumia  muda  wao   kutoa  mafunzo   ya  ujasiriamali  kwa  wajasiriamali  wadogo  wadho  waliopo  maeneo  ya  vijini  nchini  Tanzania.

                                     BAADA  YA  MAFUNZO
Baada  ya  mafunzo,   vijana  watakao  pata  nafasi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  na  kufuzu  vizuri  watapewa  nafasi  ya  kufanya  kazi  na  asasi  kama  wawezeshaji  ama  walimu  wa  mafunzo  ya  ujasiriamali   katika  maeneo  ya    vijijini  ambako  muhusika  atapangiwa  na  asasi.

                                      KUHUSU  MRADI
Mradi  wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Vijijini  ni  mradi  unao  ratibiwa  na  kusimamiwa  na  asasi  ya   RafikiElimu  Foundation  kwa  msaada  wa   mashirika  mbalimbali.   Dhumuni  la  mradi  ni  kutoa  elimu  ya  ujasiriamali    kwa  wajasriamali  wadogo  wadogo   wapatao  5000  waliopo  katika  maeneo  ya  vijijini  nchini  Tanzania  kwa  kuwatumia  vijana  wa  kitanzania  waliopata  mafunzo  ya  kuwawezesha   kufanya  kazi  kama  walimu  wa  ujasiriamali.

MAOMBI  :   Tuma  barua  yako  ya  maombi , ambatanisha  na  C.V yako,  nakala  ya  cheti  chako  cha  kuzaliwa  ama/  nakala  ya  kadi  ya  mpiga  kura, pamoja  na  nakala  ya  risiti  ya  malipo  ya  ada  ya  mafunzo  kwenda   kwa  :

Meneja  Mradi,
Elimu  Ya  Ujasiriamali  Vijijini
c/o  RafikiElimu   Foundation,
S.L.P   35967,
Dar  Es  salaam.

Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  10   Agosti  2012. .
Kwa  maelezo  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu :  0714728415  au 0763976548 

Wateja wa Airtel sasa kutuma pesa Bure kupitia Airtel money

   Kupata huduma ya Airtel money  sasa piga *150*60# Bure

 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa  muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure  

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu kirahisi zaidi  nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma  na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa  na mengine mengi

tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60#   na kuunganishwa moja kwa moja

vilevile  tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha  wateja wetu wote na wakala  wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii  iliyorahisi ni rahisi aliongeza” Mmbando

Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha  na kusaidia wateja wetu kuokoa muda  kwenda mbali kupata huduma za kibenki.

Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa , kununua salio na huduma nyingine nyingi

Rais Kikwete ahudhuria mazishi ya shemeji yake mjini Lindi leo

Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi leo Julai 30, 2012.PICHA NA IKULU 
Rais Kikwete akishiriki katika swala ya kumuombea marehemu mjini Lindi leo Julai 30, 2012.Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Julai 30, 2012 amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi (45),  aliyefariki Jumamosi iliyopita jijini Dar es salaam, na kuzikwa katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.

Mkurugenzi wa msama promotions,alex msama akizungumza na waheshimiwa mapema leo mjini dodoma.

Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd.Bwa. Alex Msama akizungumza jambo  na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Mizengo pinda mapema leo nje ya jengo la Bunge mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd.Bwa. Alex Msama akizungumza jambo  na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia mapema leo nje ya jengo la Bunge mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd.Bwa. Alex Msama akizungumza jambo  na Naibu Waziri wa  Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Amos Makalla mapema leo nje ajengo la Bunge mjini Dodoma. 

Mke wa waziri mkuu,Mama Tunu Pinda azindua MRADI WA MAJI KATIKA HOSPITALI YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO.

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifungua pazia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Richard Wells anaemaliza muda wake ikiwa ni sehemu ya ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi mjini Moshi, mradi huo ambao umefadhiliwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL umegharimu zaidi ya milioni 50 za kitanzania uliolenga kutoa suluhisho la muda mrefu katika matatizo sugu yanayoikumba jamii hususani tatizo la uhaba wa maji safi kwa maendeleo ya maisha ya mtanzania, Kushoto katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk Msengi,Aidha Matanki hayo yana uwezo wa kuhifadhi lita za maji elfu 40.000 kwa wakati mmoja.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Richard Wells anaemaliza muda wake kwa kazi nzuri iliyofanywa na kampuni yake ya SBL. Kushoto pichani ni  Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk Msengi.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda pamoja na Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon wakifungua bomba  la maji mara baada kuzinduliwa rasmi mradi huo kwenye hospitali ya Mkoa ya Mawenzi mjini Moshi leo, wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk Msengi na kushoto ni Mkurugenzi wa Serengeti SBL aliyemaliza muda wake Bw. Richard Wells.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano kampuni ya SBL,Teddy Mapunda akitoa ufafanuzi mfupi mbele ya mgeni rasmi katika uzinduzi huo,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda pichani kulia akisikiliza kwa makini,shoto ni Mkurugenzi wa SBL anaemaliza muda wake Bw. Richard Wells.
Mkurugenzi wa kapumpuni ya SBL anaemaliza muda wake Bwa.Richard Wells akisoma hotuba yake kwa ufupi mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa mradi wa maji kwenye hospitali ya Mwanzi,ambapo kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa kapumpuni ya SBL anaemaliza muda wake Bwa.Richard Wells akikabidhi hotuba yake kwa Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda.
Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, amesema mradi huo uliogharimu zaidi ya milioni 50 za kitanzania ulilenga kutoa suluhisho la muda mrefu katika matatizo sugu yayoikumba jamii hususani tatizo la uhaba wa maji safi kwa maendeleo ya maisha ya mtanzania.

“sisi kampuni ya bia ya Serengeti tunatambua sana changamoto zinazowakabili watanzania, taasisi na mashirika mbalimbali hususani hospitali juu ya upatikanaji wa maji safi na salama, na kwasababu hiyo kampuni ya bia ya Serengeti imeona hilo na kuamua kusadia kutatua tatizo hilo katika maeneo mbalimbali ikianza katika maeneo yanayohitaji huduma ya maji kwa haraka zaidi” alisema Mapunda na kuongeza kuwa kujitolea kusaidia jamii ni moja yab sera za kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kurudisha shukrani zake kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL,Teddy Mapunda kikabidhi hotuba yake kwa Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda.Pichani mwisho kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh Leonidas Gama. 
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Bwa. Ephraim Mafuru akizungumza jambo mapema leo kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa maji,ambapo Mradi huo umezinduliwa leo na mke wa waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania Mama Tunu Pinda akiwa ndio mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambapo katika kuuzindua mradi huo uliopata kuhudhuriwa na waandishi wa habari,maafisa kutoka ngazi mbalimbali serikalini mkoani hapo na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro. 
Mke wa waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania Mama Tunu Pinda akipanda mti kwenye moja ya kiunga cha hospitali hiyo ya   Mawenzi,shoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL,Teddy Mapunda 
Mke wa waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania Mama Tunu Pinda pichani kati akipanda mti kwenye moja ya kiunga cha hospitali hiyo ya   Mawenzi,shoto ni Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akizungumza katika uzinduzi huo huku wakuu wa kampuni ya bia ya Serengeti wakimsikiliza kwa makini, kutoka kushoto ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa SBL Bw. Steve Gannon na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake Richard Wells na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Leonidas Gama.Katika hafla hiyo,Mama Pinda huku akiwataka wakazi na watumiaji wa hospitali ya mawenzi mkoani Kilimanjaro na watanzania kwa ujumla kujenga imani na mahusiano mazuri na makampuni binafsi hasa yanayojali wateja wake na wananchi kwa ujumla kama kampuni ya bia Serengeti.

“Ni mwezi mmoja sasa umepita tangu kampuni hii hii yani Serengeti Breweries ilipozindua mradi mkubwa sana wa maji huko mkoani Iringa na ndio maana nawapongeza sana kwamba mnawajali na kuwasaidia watanzania bila kubagua, najua kuwa mliwahi kujenga mradi mkubwa wa maji Mkuranga jiji Dar es Salaam na kwa sababu hiyo sasa ifike mahali jamii ya watanzania waamini na kutambua kuwa kuwepo kwa kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchi kumeleta faida kubwa kwa sereikali na kwa jamii hongereni sana Serengeti breweries kwa juhudi zenu za dhati kabisa za kuinua uchumi ya watanzania” alisema mama Pinda.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Leonidas Gama akizungumza kwa ufupi kwa madhumuni ya kumkaribisha mgeni rasmi,Mama Tunu Pinda.
Kutoka kulia ni Mganga mkuu wa Mkoa wa Kiliamjaro Dk Mtumwa Mwako Mkurugenzi Mtendaji mpya wa SBL.Bwa. Steve Gannon, Mkurugenzi Mtendaji anaemaliza muda wake,Bwa.Richard Wells pamoja na Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano Bi.Teddy Mapunda wakimsubiri mgeni rasmi.
Kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Miradi  Endelevu na uwajibikaji Bw. Malisa, Imani Lwinga Meneja Mawasiliano na Mtaalamu Masuala ya Fedha SBL Bw. John Collins.
Baadhi ya wauguzi na wahudumu wa hospitali ya Mawenzi wakishuhudia tukio hilo mapema leo.Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.

Mradi huo umezinduliwa leo na mke wa waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania Mama Tunu Pinda akiwa ndio mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambapo katika kuuzindua mradi huo uliopata kuhudhuriwa na waandishi wa habari,maafisa kutoka ngazi mbalimbali serikalini mkoani hapo na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro.

Mama Pinda alielezea kufurahishwa kwake na juhudi zinatofanywa na kampuni ya bia ya Serengeti katika kuisadia jamii ya watanzania bila kupendelea upande wowote. 

serikali laifungia gazeti la mwanahalisi kwa mda usiojulikana


GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA.

            Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

            Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

            Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
            Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
          
  Uamuzi wa Serikali

            Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.

             Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

            Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia  taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.

            Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.
Imetolewa na

OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
30 Julai, 2012

WATER PROJECT COMMISSIONING FOR MAWENZI HOSPITAL IN MOSHI.

July 30, 2012 Serengeti Breweries Limited today commissioned a project of over 55mil to the Mawenzi Hospital in Kilimanjaro region.  This project consists of a big water storage tank for this hospital. The facility was commissioned by Hon. Mama Tunu Pinda as the guest of honour, the wife of the Prime Minister.

Speaking at a brief ceremony on the site, she acknowledged, “I am glad that this facility will provide the community with the much-needed resource and wish to thank SBL and EABL Foundation for their efforts.” She further revealed that the project would go a long way in reducing the impact of water borne diseases which was prevalent in the fast expanding area. 

Speaking to the journalists during the launch, Mama Pinda expressed her gratitude to SBL for recognizing the importance of water in the public sector including schools and hospitals. “I am aware of the recent Iringa project. Another facility costing approximately TZ 50 Million has been constructed through funding of EABL Foundation and Serengeti Breweries Limited (SBL) and will benefit over 150,000 people, from the bottom of my heart and on behalf of the people of Tanzania I want to say Thank you’.

The Corporate Relations Director for Serengeti Breweries Limited, Teddy Mapunda, said that SBL was committed to work with community especially hospitals in providing long term and sustainable solutions through provision of clean, sustainable water sources as a way of giving back to the community.
“As a company, SBL recognizes that water is a basic need and an important catalyst for both economic and social development of the country. Finding sustainable solutions to the problems of our people underscores our commitment to the communities in which we operate” said Mapunda adding that  last year, SBL/EABL Foundation commissioned water and sanitation project in Mkuranga and was part of corporate companies and NGO’s that came together to improve water at Amana hospital in Dar es salaam. “Serengeti Breweries Limited and EABL foundation invested 384.6 Million on Mkuranga Water project to benefit more than 250,000 people” she added. 

 
Nafasi Ya Matangazo