Thursday, September 20, 2012

Rais wa zanzibar Dkt shein ateua manaibu makamu mkuu wa suza


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein  amefanya uteuzi wa Manaibu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA).
 
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Zanzibar DKT. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa DKT Shein amemteuwa DKT.Zakia Mohammed Abubakar kuwa Naibu Makamo Mkuu wa SUZA ataeshughulikia masuala ya Utawala.
 
Pia DKT Shein amemteuwa DKT Haji Mwevura  kuwa Naibu Makamo Mkuu wa Chuo hicho atakaeshughulikia  masuala ya Taaluma.
 
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa  chini ya kifungu10(1)cha Sheria ya SUZA namba 8 ya mwaka 1999 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha 4 cha Sheria namba 11 ya mwaka 2009.
 
Uteuzi huo  umeanza leo.
 
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
20/9/2012

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.