Wednesday, August 1, 2012

Mwanasiasa Mkongwe Hassan Nassor Moyo amewataka wananchi wa Zanzíbar kuzungumzia suala zima la mustakbali wa nchi na sio kuchanganya mambo

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar    01/08/2012.

Mwanasiasa Mkongwe  Hassan Nassor  Moyo amewataka wananchi wa Zanzíbar  kuzungumzia suala zima la mustakbali wa  nchi  na  sio kuchanganya mambo   kwani nchi ni mali ya wananchi hivyo wanahaki ya kusikilizwa nini  wanataka.



Amesema  chama  kinaweza kuwepo na kuondoka lakini  nchi haiondoki hivyo wananchi wapewe fursa ya kuzungumzia  suala la nchi yao  na mambo wanayotaka kubadilishwa katika Muungano  bila ya ugomvi wala fujo .

Hayo aliyasema leo huko katika ukumbi wa Rumaisa  karibú na Hoteli ya Bwawani  wakati akizungumza  na waandishi wa habari wa vyombo  Mbali Mbali , wanafunzi wa chuo kikuu,pamoja  na wananchi waliofika hapo .
  
“Siwezi kupinga Muungano hata mara moja lakini Muungano tuubadilishe,” alisema, Moyo . 
Aidha alisema  ili kuimarishwa  Muungano  ni lazima ufanyiwe marekebisho  ya kasoro  zinazojitokeza zirekebishwe kwa furaha na  sio kwa chuki na jazba .

“Tuzungumzie muungano kwanza katiba mwisho , tunataka uhuru wa kujitawala wenyewe sio kutawaliwa,”alisema Moyo. Alidai kuwa wananchi   wengi wanasema hawautaki Muungano uliopo hivi sasa wanataka muungano ambao utaendana na wakati uliopo.
  
Aidha alifahamisha kwamba kuna baadhi ya  kasoro ambazo zilijitokeza  kabla ya Marehemu Karume ziliambiwa kwamba kurekebishwa bado haijafika wakati wake sasa wakati  ndio huu  wakurekebisha kasoro hizo.

Hassan Nassor Moyo ambaye anatokea katika vyama vya Wafanyakazi Zanzíbar  alishika nyadhifa  Mbale Mbale katika Serikali ya Mapinduzi na ya Jamhuri ya  Muungano  wa Tanzania. 

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

perfect mzee nyinyi ndio icon ya kutetea Watanganyika wapewe nchi yao na Zanzibar iwe huru,Swali langu Kwa nini Tanganyika hamtaki kurudishiwa nchi yenu? Wazanzibari tunajitahidi muwe na nchi lakini nyie hamuitaki? au mnataka Tanzania yote iitwe ZANZIBAR?Mnalipenda jina nini?