Wednesday, August 1, 2012

habari za hivi punde: Ngassa atua simba kwa milioni 25 .?!

Na Mahmoud Zubeiry

MRISHO Khalfan Ngassa ameuzwa Simba kwa dau la Sh. Milioni 25 mchana wa leo, Azam imethibitisha.

Habari za ndani kutoka Azam, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka klabu hiyo, zimesema kwamba Simba wamelipa fedha hizo na wamesainiwa fomu za uhamisho na sasa Mrisho anafuata nyayo za baba yake Khalfan Ngassa, ambaye aliichezea Simba SC 1991/1992. 

Azam ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya mchezaji huyo iliyemsajili kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya Yanga baada ya kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Na uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo.Kwa habari zaidi Chimbua Hapa.

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

hayo ndiyo matatizo ya kuendekeza ushosti kwenye mpira.huu urafiki gani ambao mara zote simba tu ndio wanaofaidika badala yaazam.hili dili lilishapangwa na lile tagazo la kumuuza lilikuwa danganya toto.kwanza huyo kahemela nui shabiki mkubwa wa simba .haya tutaona huo mkataba wa ngassa na simba utakavyokuwa ,kwani suala la mkataba azam hawana nafasi tena