Wednesday, August 22, 2012

ccm yaamua kukata rufaa kufuatia kutenguliwa kwa matokeo ya jimbo la igunga


Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora.

Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu. Kusudio hilo linatokana na kutoridhishwa na hukumu hiyo.

Imetolewa na;-

Nape Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM
WA
ITIKADI NA UENEZI
22/08/2012

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

 
Nafasi Ya Matangazo