Friday, August 10, 2012

Airtel yapeleka Kikosi cha wachezaji nyota wa Airtel Rising Stars Nairobi.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jackson Mmbando(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kikosi cha timu ya Airtel Rising Stars kinachokwenda kushiriki michuano ya Inter-continental itakayofanyika Nairobi, Kenya baadaye mwezi huu. KAtikati ni Afisa Habari wa kampuni hiyo Jane Matinde na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA).
Afisa Habari wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jane Matinde(kushoto) akizungumza na waadishi wa habari wakati wa kutangaza kikosi cha timu ya soka cha Airtel Rising Stars kitakachoshiriki michuano ya Inter-continental yatakayofanyika Nairobi, Kenya mwezi  huu. Amefuatana na na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando(kulia)

=======   =======   =======

Airtel yapeleka Kikosi cha wachezaji nyota wa Airtel Rising Stars Nairobi
.       Timu ya Yoso bora 16 kuwakilisha Tanzania kwenye michuano ya
Airtel Rising Stars  Afrika

Dar es Salaam, Airtel Tanzania kupitia mpango wake maalum wakuvumbua
na kukuza vipaji vya soka nchini ujulikanao kama Airtel Rising Stars
leo wametangaza kikosi cha wachezaji 16 watakaoiwakilisha Tanzania
kwenye mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Airtel yatakayofanyika Nairobi kuanzia Agosti 19 hadi 25, 2012.

Wachezaji hao walichaguliwa na jopo la makocha kwa kushirikiana na
shirikisho la mpira TFF na chama cha mpira cha Dar es Saalam DRFA
wakati wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika kwenye
uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam mwezi Juni na
kushirikisha timu kutoka mikoa ya Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Temeke
na Kinondoni.

Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za TFF leo, Afisa
Maendeleo wa mpira wa miguu nchini Salum Madadi aliwataja vijana
watakaowakilisha Tanzania kuwa ni Denis Richard, Juma Hamza, Abdul
Selemani, Ishaka Shekolowa na Bakari Ally kutoka mkoa wa kisoka wa
Temeke.

Wengine ni Abdulatif Mohamed, George Joseph na Badilu Said (Lindi),
Said Kassim, Amos Ikungula, Paul Balama na Goodluck Mabiku (Ilala),
Joel Kasimula na Ibrahim Mtenga (Mbeya), Sntkony Angelo na Suleiman
Yunus (Arusha).

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkali yatashirikisha
wachezaji wengine nyota wa ARS kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi,
DRC, Congo Brazzaville, Nigeria, Ghana, Zambia, Niger, Gabon, Burkina
Fasso, Sierra Leone, Chad, Madagascar na Tanzania.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya
amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kimataifa ni kuwapa vijana
fursa zaidi ya kuendeleza vipaji vyao na kupata uzoefu. "Vile vile
Airtel Rising Stars inatoa nafasi kwa wanasoka hawa chipukizi kuweza
kupanua jiografia yao na kujenga urafiki na vijana wenzao kutoka nchi
mbali mbali", alisema Singano.

Michuano hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo pia
itafanyika Nairobi chini ya walimu wa soka la vijana kutoka klabu
maarufu duniani ya Manchester United ya Uingereza. Kliniki kama hii
ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa kisasa wa soka jijini Dar es
Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya, Malawi, Sierra Leone na
wenyeji Tanzania.

Katika kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji sita
miongoni mwao ni wavulana watatu na wasichana watatu ambao walioibuka
kuwa wachezaji bora wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam
mwezi Juni.

Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza vipaji vya
wanasoka wanaochipukia barani Afrika. Walengwa ni wavulana na
wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata fursa
ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya waatalum wa mpira wa miguu
wa kitaifa na kimataifa.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.