Saturday, July 28, 2012

yanga yatwaa kombe la kagame 2012,yainywesha azam cola 2-0

Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia na kombe lao walilokabidhiwa leo mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika mchezo uliokuwa wa kusisimua kwa kiasi kikubwa,pamoja na kuwepo kwa msisimko mkubwa, timu ya Yanga waliinywesha timu ya Azam cola 2-0 kwenye mchezo wa fainali katika michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Askari wa usalama a.k.a akina Ras Makunja wakihakikisha usalama wa kutosha unakuwepo uwanjani hapo jioni ya leo
 Mbwembwe za shabiki wa Azam FC
 Unazi wa mpira wa miguu kazi kweli kweli.
 Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa wamemwagika vilivyo uwanja wa Taifa jioni ya leo.
 Shabiki wa Yanga na mbwembwe zake kama hivi.
Wadau wakiinasa  picha ya makocha wa timu ya Azam na Yanga walipokuwa wakijadiliana jambo  kabla ya mchezo kuanza jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa,jijini Dar.
 Hatari kwenye lango la Yangaaaa....!
 Mwali aliyechukuliwa na timu ya Yanga.
 Mashabiki wa mpira wakiwemo na wa timu ya Azam FC wakifuatilia kwa makini kandanda safi kabisa.
Maafande wakiwamtuliza mtu mmoja ambaye hakujulikana jina lake mara moja,wakati fujo zilipotokea eneo hilo.

=======   ======  =====  ====

Habari kwa hisani ya Prince Akbar 

YANGA ya Dar es Salaam imetwaa Kombe la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0.

Yanga sasa imebakiza mara moja kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba kutwaa Kombe hilo, mara tano kwa sita. Yanga ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012. Mashujaa wa Yanga leo walikuwa Hamisi Kiiza aliyefunga bao la kwanza dakika ya 44 na Said Bahanuzi aliyefunga la pili dakika ya tatu ya muda nyongeza, baada ya kutimu dakika 90 za mechi hiyo.

Kiiza alifunga bao lake, baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kumpiga chenga kipa huyo kisha kuusukuma mpira nyavuni. Bahanuzi aliuwahi mpira mrefu uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa Azam kabla ya kumtungua Dida.

Mechi hiyo imechezeshwa vema na refa Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi, akisaidiwa na Simba Honore wa Rwanda na Peter Sabatia wa Kenya, wakati mezani atakaa Issa Kagabo wa Rwanda, Kamisaa Hassan Amir wa Somalia na Mtathmini wa marefa ni Anangwe Robert wa Kenya. 

Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo/Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende.

Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Jabir Aziz, Kipre Tcheche/Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’. Benchi; Mwadini Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Gaudence Mwaikimba.

Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika ya 67, wakati la kufutia machozi la timu ya jeshi la Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya 89.  

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.