Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo kulia akitangaza rasmi washindi wa droo ya 11 mara baada ya kuchezesha droo hiyo, katikati ni Tumainieli Malisa kutoka PWC na kushoto ni Bakari Maggid kutoka Bodi ya taifa ya bahati na sibu.
Meneja wa bia ya Serengeti lager Allan Chonjo kulia akiongea na mmoja wa washindi wa droo ya 11 ya promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini, katikati ni Tumainieli Malisa kutoka PWC, na kushoto ni Cheryl Vroom kutoka PWC. Droo hiyo ilifanyika katika ofisi za kampuni hiyo maeneo ya oysterbay jijini Dar leo.
====== ===== ====== ======= ======
WASHINDI WENGINE WAWILI WACHOMOKA NA ZAWADI ZA SBL.
Ni wiki ya 11 sasa tangu kuanza kwa promosheni inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ijulikanayo kama ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na Serengeti Breweries Limited’ ambapo leo asubuhi, ilichezeshwa tena droo ya 11 katika ofisi za kampuni hiyo Serengeti Breweries Limited zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo wawakilishi wa kampuni ya kuendesha michezo ya kubahatisha ya Push Mobile, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Watanzania wengi wamekuwa wakishihjudia kampuni ya bia ya Serengeti ikitangaza washindi pamoja na kuwakabidhi zawadi zao kwa wakati ambapo mwishoni mwa wiki ilyopita kampuni hiyo ilikabidhi bajaj na pikipiki zote mpya kwa washindi wa zawadi hizo hapa jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika hafla hiyo, meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo, amesema kwamba“ wishoni mwa wiki iliyopita zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wetu liliendelea hapa jijini Dar es Salaam ambapo tuliwa kabidhi bw. Richard Mbezi zawadi ya Bajaj na Mbaraka Adam alikabidhiwa pikipiki mpya kabisa” alisema Chonjo na kufafanua kuwa bado zawadi ni nyingi za kushindaniwa hadi promosheni hiyo itakapofika kikomo takribani siku chache zijazo .
Washindi wa leo ni pamoja Inocent Paul 25 kutoka Morogoro ambaye amejishindia pikipiki naMwita Nyamahemba 23 kutoka Nyakato Mwanza mwanafunzi wa chuo Tarime TTC, aliyejinyakulia jenereta mpya” alisema Chonjo huku akisisitiza kuwa promoshenihiyo bado inaendelea kwa wiki takriban sita zijazo na kuwataka watanzania wote wenye sifa zilizoainishwa katika vigezo na masharti ya promosheni hiyo kushiriki kwa wingi ili kuongeza uwezo wakushinda zawadi mojawapo.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ Na kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.




Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment