Mama Maria Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa filamu.
Mama Maria Nyerere akionesha filamu hiyo aliyokabidhiwa na msanii wa filamu Steve Nyerere. Mama Maria Nyerere akisalimiana na muigizaji nyota wa filamu,Steve Nyerere.
Mama Maria Nyerere akisalimiana na mmoja wa wasanii wa filamu mahiri hapa nchini,Jacob Steven. Steve Nyerere akikabidhi filamu yake kwa Mama Maria Nyerere kama sehemu ya shukrani.
Mama Maria Nyerere akizungumza na baadhi ya wasanii wa filamu nyumbani kwake.
Mama Maria Nyerere akiwa na baadhi ya wasanii wa filamu hapa nchini.
Baadhi ya wasanii wa filamu wakiwa nyumbani kwa Mama Maria Nyerere
Mwigizaji wa filamu nchini Stive Mangele 'Steve Nyerere jana alikuwa anakabidhi filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa Mama Maria Nyerere ikiwa kama shukrani zake, baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama. Stive alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi.
Amesema Mama Maria Nyerere alimsaidia sana katika kumuonyesha vitu gani mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda, na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambapo walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo ili ikamilika.



Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment