Na Joseph Malembeka, Morogoro.
WANANCHI wilayani Morogoro wamesema Mfuko wa Bima ya Afya (CHF) hauna manufaa kwao badala yake upo kwa ajili ya kuwanufaisha wakubwa serikalini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na jopo la waandishi wa habari na mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) lililotembelea kata ya Mkambarani, baadhi ya wananchi hao, Hadija Chasamba na Mohamedi Nonzo walisema kutokana na kutopata huduma kama ilivyokusudiwa wameamua kutochangia.
Maelezo hayo yaliyoungwa mkono na baadhi ya viongozi wakiwemo madiwani Daniel Shawa, Telesia Sanga na Muuguzi mfawidhi wa kituo cha Afya Mkamabarani, Grace Mfungeni, wakisema wameshindwa kuendelea kuchangia CHF kutokana na kuambulia dawa za Asplini na Panado. “Kwanza hatujui faida za mfuko huu, tuliambiwa ukichanga sh 5,000 utawanufaisha wanafamilia 10 kupata tiba lakini ukiugua utalipia kuonana na daktari, vipimo na dawa tunajinunulia…sijaona faida ya mfuko,” alifafanua Nonzo mkazi wa Kizinga.
Mbali na CHF wanachi hao waliongeza kuwa serikali imekuwa ikiwandanganya kuwa wazee, wanawake wajawazito na watoto watapata huduma bure jambo ambalo halitekelezwi badala yake wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa huduma za msingi za afya. Wakifafanua juu ya hatua zinazochukuliwa kuboresha huduma ya afya katika kata hiyo, viongozi hao walibainisha kuanza ujenzi wa chumba cha maabala na nyumba za wahudumu wa afya.
Naye ofisa matekelezo wa CHF Kanda ya Pwani, Hamidu Mwambungu, mbali na kukiri kuwpo kwa changamoto mbalimbali kwenye utekelezwaji wa makusudio ya mfuko aliwashauri wananchi kujiunga kwa wingi na mfuko huo kwa afya bora.Chanzo Hapa.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment