Friday, June 29, 2012

Tigo kuukaribisha msimu wa Sabasaba kwa shangwe.

Edward Shila , Mtaalam wa Promosheni Uhusiano na Udhamini wa kampuni ya Tigo, akiwataarifu waandishi wa Habari juu ya tamasha la  'Tigo Sabasaba' litakalofanyika katika ufukwe wa bahari wa  Coco mwishoni mwa wiki hii, kushoto kwake ni mchekeshaji ajulikanaye kwa jina la Wakuvanga kutoka kundi la Ze Comedy na Afisa Uhusiano wa Tigo , Alice Maro.

Msanii Wakuvanga akitoa vichekesho vyake vya mama Bele kwa waandishi wa habari na pembeni yake ni Edward Shila, Mtaalam wa Promosheni Uhusiano na Udhamini wa Kampuni ya Tigo  na Alice Maro, Afisa Uhusiano wa Tigo wakifurahia kichekesho hicho.hie


=====  =====  =====
Tigo kuukaribisha msimu wa Sabasaba kwa shangwe.

Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo itawasha moto mwisho wa wiki hii ikisindikizwa na baadhi ya wasanii watakaotoa burudani katika fukwe za bahari. Maadhimisho haya ya siku mbili,  ambayo ni mwanzo wa maonyesho ya biashara ya Sabasaba, utafanyika katika ufukwe wa bahari ya Coco Jumamosi, Juni 30 na Jumapili Julai 1, 2012 kuanzia saa 5 asubuhi hadi 12 jioni.Tumia nafasi hii kupima uwezo na vipaji vyako katika kuimba, kucheza na sarakasi katika  mashindano ya Tigo ya kusaka vipaji vya chipukizi yaliyoandaliwa kwa watakao hudhuria. Au unaweza kukaa na kuburudika pamoja na wanamuziki Mr. Nice na H Baba wakitumbuiza.

“Mwakahuutumeamuakuwaleteaburudaninyingizakutosha”, alisema Alice Maro, AfisaUhusianowaTigo. “  Hatutotaka wateja wetu waje tu kufurahi mwisho wa wiki hii ila tungependa pia wapate fursa ya kupata huduma zetu bora na nafuu zilizoandaliwa kwa ajili yao” alisema.

Kilele cha maadhimisho kitakuwa Jumapili na burudani kutoka kwa Juma Nature, Roma Mkatoliki, Izzo B, Professor Jay, Mwasiti, Barnabas,Fid Q, Joe Makini na burudani maalum kutoka kundi la wachekeshaji la “Ze Comedy”.

Hakutakuwa na sababu za kuondoka jua likizama kwani maadhimisho yatamaliziwa na fainali za EURO mwaka 2012. Fainali hizi zitaoneshwa katika skrini kubwa kuanzia saa mbili usiku. Kiingilio ni bure naTigo inawahamasisha wote kufika katika ufukwe wa bahari ya coco ili kusherekea na kuukaribisha msimu wa Sabasaba.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.